Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Fatma Almasi Nyangassa amepiga marufuku shughuli zote za uchimbaji wa vifusi katika machimbo yaliyopo katika mtaa wa Mjimwema
Mheshimiwa Nyangassa ametoa kauli hiyo mchana wa leo alipotembelea eneo ilipotokea ajali ya watu kufukiwa na kifusi iliyotokea siku ya jumapili ambapo watu 3 walipoteza maisha.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya ametoa muda wa siku tatu hadi kufukia jumamosi tarehe 09/04/2022 Wananchi wote wa eneo la machimbo kutoa mali zao zote na baada ya hapo ukaguzi utafanyika kuhakikisha eneo hilo linabaki salama.
Sambamba na hilo amewataka wananchi wote kuacha tabia ya kuuza kokoto barabarani na kuacha kuchimba vifusi hovyo hovyo ili kueupuka uharibifu wa mazingira ikiwa pamoja na kufuata maelekezo wanayopewa na Wataalamu.
Aidha Diwani wa Kata ya Mjimwema Mheshimiwa Omary Ngurangwa amesema kuwa eneo hilo si salama kwa shughuli ya uchimbaji na serikali ilishatoa maelekezo kuwa eneo hilo lisitumike.
Naye bwana Ally Maganga ambaye ni Afisa Madini wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa hakuna biashara au liseni yoyote ya uchimbaji katika eneo hilo na amewataka Wananchi wanao taka kuchimba vifusi kuhakikisha wanapata liseni kutoka mamlaka husika
Wananchi wakimsikilizaMMkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Fatma Almasi Nyangassa.
Mwananchi akitoa ombi la kutafutiwa eneo rasmi la uchimbaji wa vifusi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa