Wananchi wa Kigamboni wazidi kutahadharishwa kuchukua tahadhari na kuondoka kwenye maeneo hatarishi kabla ya kipindi cha mvua kuanza ili kuepuka madhira yatakayoweza kuwakumba kutokana na mafuriko.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya leo Bi.Rahel Mhando (Katibu Tawala) wakati wa kikao cha baraza la madiwani amesema kuwa Mkuu wa Wilaya mbali na kutoa pongezi kwa watendaji na waheshimiwa madiwani kwa utendaji kazi, ameto rai kwamba kila mmoja asimame kwenye nafasi yake katika kuhakikisha tahadhari na elimu inatolewa kwa wananchi wanaoishi mabondeni kuondoka ili mvua zitakapoanza kila mmoja awe salama.
Diwani wa Kata ya Kibada ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa Mh.Amin Sambo alisema kuwa watu wote waliojenga nje ya utaratibu wasimamiwe kufuata sheria kwasababu madhira yakitokea Manispaa itawajibika , hivyo ni suala la msingi kuwaelewesha wananchi juu ya ujenzi wa makazi kwenye maeneo ambayo ni karibu na vyanzo vya maji na mabondeni ili usalama uwepo pande zote.
Naye diwani wa kata ya Kimbiji Mhe. Bunaya Sanya amesema kuwa Kigamboni bado inakua na maeneo mengi yapo wazi hivyo hakuna sababu ya wananchi kujenga kwenye maeneo hatarishi wakati yapo maeneo mazuri ambayo wanaweza kujenga na kuisha kwa usalama.
Aidha Baraza limeridhia na kumtaka Mkurugenzi kuunda timu ya wataalamu watakaopita na kuanisha maeneo yote hatarishi na vyanzo vya maji ili kuwakataza wananchi kufanya shughuli zozote hususani ujenzi.
Wakati huohuo wakipokea taarifa ya mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa iCHF Madiwani wametaka matangazo na kampeni zifanyike ili kuweka uelewa kwa wananchi juu ya umuhimu wa bima hii na namna inavyofanya kazi sababu mfuko huu umelenga zaidi kusaidia wananchi wa hali za chini.
Katibu Tawala Wilaya Bi. Rahel Mhando akitoa salam kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Mratibu wa mfuko wa afya ya jamii iCHF Bi.Sereti Kiroya akisoma taarifa kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Mkurugenzi wa Manispaa Arch.Ng'wilabuzu Ludigija akijibu maswali ya papo kwa papo ya Waheshimiwa Madiwani
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa