Leo Julai 22, 2025,, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mheshimiwa @dalmiamikaya ameendelea na ratiba yake ya kukutana na makundi mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuhamasisha maendeleo ya wilaya hiyo.
Katika mwendelezo huo, Mh. Mikaya amekutana na viongozi wa vyama vya siasa wakiwemo wenyeviti na makamu mwenyekiti wa vyama mbalimbali. Mazungumzo hayo yalilenga kujadili namna ya kufanya siasa zenye tija, maadili na zinazojenga amani kwa ajili ya ustawi wa Wilaya ya Kigamboni.
Aidha, viongozi wa vyama vya siasa walipata fursa ya kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazokabili shughuli zao ndani ya wilaya. Mheshimiwa Mikaya amepokea kwa makini hoja na changamoto hizo, na ameahidi kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na mamlaka husika ili kuwezesha mazingira bora ya utekelezaji wa shughuli za kisiasa kwa amani na ustawi wa Kigamboni
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa