Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw. Erasto Kiwale ameiagiza Kamati ya Lishe katika manispaa hiyo kuwa na mikakati madhubuti ya kutimiza malengo ya mwaka na kuwa na viashiria vya kupima utekelezaji wake.
Bw. Kiwale ameyasema hayo Agosti 14, 2025 katika kikao cha Kamati ya Lishe kilichafanyika Ukumbi wa Mikutano, Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.
“Tunapoweka malengo tuweke na namna ya kujipima, ili tunaporudi kupitia malengo haya tuwe na sehemu ya kufanya rejea, kupitia hivyo tunaweza kujua tumefanikiwa/hatujafanikiwa kwa kiasi gani, hapo tunaweza kuwa na mikakati bora ya kuhimili changamoto” amesema Bw. Kiwale
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa