"Naomba nitoe rai kwa Wananchi wa Kigamboni na maeneo mengine, sote tunajukumu kubwa la kuhakikisha tunavilinda vyanzo vya maji kwani maji ni sisi na sisi ni maji pia maji ni Mazingira"
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila leo Septemba 2023 katika ziara yake ya kukagua na kujione changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya uwekezaji ndani ya Manispaa ya Kigamboni.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amesema Serikali inatambua umuhimu wa upatikanaji wa maji kwani yanamchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi kwasababu viwanda vingi hutegemea maji katika kujiendesha na kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo huuzwa ndani na nje ya nchi hivyo kuiwezesha nchi kupata Kodi pamoja na fedha za kigeni
Kwa upande mwingine ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka Mkoa wa Dar es Salaam DAWASA kwa kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Wananchi wanapata maji ya uhakika.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa