Wilaya ya Kigamboni imefanya uzinduzi wa ushirikishaji wananchi na wadau mbalimbali kwenye utoaji wa maoni wa namna wanayohitaji kigamboni iwe, kwenye maandalizi ya mpango kabambe yaaani Kigamboni Master Plan unaolenga kuupanga mji wa Kigamboni na kuiinua Wilaya Kiuchumi na Utoaji wa huduma za kijamii ili iweze kuleta tija kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa utoaji wa maoni kwenye ukumbi wa Islamic Club jana Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri amesema Mradi wa Mpango Kabambe umelenga kuboresha mapungufu yaliyojitokeza kwenye New Kigamboni City ulionzishwa 2008 hivyo lengo la kushirikisha wananchi na wadau mbalimbali limelenga kuiona Kigamboni ya sasa na nini ambacho kinaweza kuwekwa kuibadili Kigamboni kwenye hali ya Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni.
“Asilimia 89 ya wananchi wanaoishi kigamboni wapo kwenye ajira binafsi ambazo ni shughuli ndogo ndogo kwaajili ya kujikimu na hivyo kuifanya Kigamboni kuwa ni Makazi, hakuna uzalishaji unaoweza kuinua uchumi wa Kigamboni, ukuaji wa kipato kigamboni kipo chini na huduma za msingi za kijamii hazijitoshelezi, hivyo mpango huu na ushirikishwaji unaofanyika utawezesha kuiboresha Kigamboni”.
Akizungumzia lengo la mradi wa Mpango Kabambe Dk.Victoria Mwakalinga mtaalamu kutoka chuo kikuu cha ardhi alisema kuwa Mkutano umelenga kupokea taarifaya hali ya sasa ya kigamboni, kujadili na kutoa maoni ya kuiboresha, kujadili changamoto na fursa za kimipango miji zilizopo kigamboni ili kuzitumia katika uandaaji wa mpango enedelevu, kuandaa rasimu ya maono ya Manispaa ya Kigamboni katika kipindi cha miaka 20-30( Je ni aina gani ya mji wa Kigamboni watu wanautaka?), kutengeneza rasimu ya vipaumbele vya maendeleo na kuibua na kujadili wadau muhimu wa maendeleo ili kufanikisha utekelezaji wa mpango.
Mradi wa mpango kabambe umelenga kuupanga mji wa kigamboni na kuepuka makazi holela, kuibua na kuiweka miradi ya maendeleo itakayochochea ukuaji wa Mnaispaa ya Kigamboni katika mpango endelevu, kutoa mwongozo wa kuendeleza kila kipande cha ardhi ndani ya mji ili kuitumia ardhi kwa ufasaha, kutafuta wawekezaji na wadau mbalimbali wa maendeleo, kuainisha mipango ya sasa na ijayoya idara zote zinazofanya kazi katika Manispaa na kushughulikia kero zote za wananchi kuhusiana na mausuala ya mipango miji.
Mradi wa Mpango Kabambe unaandaliwa kwa ushirikiano baina ya Manispaa ya Kigamboni, wataalamu kutoka chuo kikuu cha Ardhi na tasisi inayoshughulikia maendeleo ya I4ID.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri akifungua jukwaa la maoni kwa wananchi na wadau mbalimbali
Dk.Victoria Mwakalinga kutoka chuo kikuu cha ardhi akielezea Mpango kabambe namna utakavyoweza kuibadili Kigamboni
mwakilishi wa Mkurugenzi na MKuu wa Idara ya Arhi Bi.Nice mwakalinga akifafanulia wananchi namna gani wanapaswa kutoa hoja ya kigamboni ipi wanaitaka iwe.
mdau akitoa maoni ya uboreshwaji wa mpango kabambe
Viongozi mbalimbali wakisikiliza kwa makini makusudi ya kuwa na mpango kabambe
Wadau na wananchi walioshiriki kwenye mkutano wa kutoa maoni juu ya mpango kabambe
wazee wastaafu wakisikiliza hoja mbalimbali zinazotolewa
wananchi wakiendelea kutoa hoja
Mwenyekiti wa wananchi akifafanua kwa wananchi na wadau nini wanapaswa kufanya kwenye mpango kabambe
wananchi wakiendelea kutoa hoja.
watumishi na viongozi mbalimbali wakifatilia hoja zinazotolewa na wananchi
Mdau wa Islamic Club akitoa hoja juu ya maboresho ya mpango kabambe
Diwani wa Kata ya Kimbiji Mhe.Sanya Bunaya akitoa hoja.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa