Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Pauline Gekul amewataka Wananchi wa Manispaa ya Kigamboni kujiajiri katika ufugaji wa Samaki ili kujipatia kipato na kukuza uchumi wa viwanda kupitia usindikaji.
Mheshimiwa Gekul ametoa wito huo katika ziara yake aliyoifanya leo ndani ya Manispaa ya Kigamboni ambapo alitembelea kiwanda cha utotoleshaji wa vifaranga vya samaki na uuzaji wa Samaki cha Big Fish kilichopo kata ya Kibada ambapo alijionea shughuli mbalimbali za uzalishaji katika kiwanda hicho.
Aidha katika ziara hiyo Naibu Waziri ametoa wito kwa Manispaa ya Kigamboni kutumia fursa ya uzalishaji wa Samaki kwa kutenga bwawa moja la samaki ambalo litakabidhiwa kwa makundi maalumu ya kinamama, Vijana na Walemavu ikiwa ni njia ya kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.
Sambamba na hilo ameahidi kutatua changamoto zinazowakabili wafugaji wa Samaki kwa kuziondoa kodi zote ambazo kero hususani katika uagizaji wa vifaa na vyakula vya Samaki vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi.
Mheshimiwa Naibu Waziri akitembelea mabwawa ya Samaki katika kiwanda
Mheshimiwa Naibu Waziri akiwasili katika kiwanda cha Big fish Kata ya Kobada
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa