Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo amewataka wananchi wa Manispaa ya Kigamboni kufanya usafi katika maeneo yao kila siku na sio kusubiri hadi usafi wa pamoja kwani ni muhimu kutunza mazingira ili kuepuka magonjwa mbalimbali ya mlipuko.
Mkuu wa Wilaya amesema hayo wakati wa zoezi la usafi wa jumamosi ya mwisho wa mwezi ya tarehe 26/08/2023 ambapo kwa jumamosi hii ulifanyika Kata ya Kibada.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema Manispaa ya Kigamboni imeona changamoto ya Vifaa vya Kufanyia usafi katika maeneo mengi ya Umma hivyo inajipanga kutatua changamoto hiyo kwa haraka kupitia kwa Afisa Mazingira.
Kwa upande mwingine ameupongeza umoja wa Madereva wa stendi kuu ya daladaka ya Kibada kwa kujitokeza kwa wingi katika kufanya usafi wa pamoja na kuwataka kuwa Mabalozi kwa wenzao wa maeneo mengi tofauti ndani ya Wilaya ya Kigamboni.
Baadhi ya Wananchi walioshiriki katika usafi Kata ya Kibada
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo akishiriki usafi wa pamoja na Wananchi wa Kibada.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa