Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili kupata fursa ya kushiriki uchaguzi ifikapo Novemba 27,2024.
Hayo ameyasema leo Septemba13,2024 wakati wa ufunguzi wa kikao chake na wananchi ik0iwa ni muendelezo wa ziara yake ya mtaa kwa mtaa iliyolenga kusikiliza na kutatua kero.
Akifafanua kaimu Mkuu kitengo cha uchaguzi bi Magdalena Malunda amesema wananchi wote watapata fursa ya kujiorodhesha kwenye daftari la wapiga kura la serikali ya mitaa kuanzia Oktoba 11-20, 2024 hivyo kila aliyetimiza miaka 18 na kuendelea ataruhusiwa kujiorodhesha na hatimage kushiriki uchaguzi ikiwemo kupiga kura.
"Orodha hii ni tofauti na orodha ya daftari la kudumu la wapiga kura inayoandaliwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi hivyo tunapaswa kujiorodhesha kwenye orodha ya wapiga kura. Alisema bi Marunda.
Aia Bi. Malunda amewataka wananchi wenye sifa za kugombea wenye umri kuanzia miaka 21 nakuendelea wajitokeze kugombea nafasi mbali mbali katika uchaguzi huo.
Kauli mbiu ya uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 inasema "SERIKALI ZA MITAA, SAUTI YA WANANCHI JITOKEZE KUSHIRIKI".
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa