Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo amewataka Wanachi wa Manispaa ya Kigamboni kula Mlo kamili wenye makundi yote 5
ya chakula ambayo ni Nafaka, mizizi na ndizi mbichi na vyakula vitokanavyo na wanyama, Mimea jamii ya kunde, Mboga za majani, Matunda, Vyakula vyevye mafuta ya mimea, Asali, pamoja na sukari ili kuimarisha Afya zao.
.
Mheshimiwa Bulembo ametoa wito huo leo Oktoba 16.2023 katika maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kiwilaya yamefanyika Mtaa wa Nyange, Kata ya Pembamnazi, Manispaa ya Kigamboni.
Aidha katika maadhimisho hayo amewataka wadau wa kilimo, ufugaji na umwagiliaji pamoja na wadau wa Uvuvi kutumia vizuri vyanzo vya maji kwa kutumia teknolojia rafiki inayowezesha kulinda na kutunza vyanzo vya maji wakati wa kuvua samaki na ulimaji wa mazao ya chakula.
Sambamba na hilo D.C amewataka Wananchi wa Manispaa ya Kigamboni kuacha kilimo cha kutegemea mvua na badala yake kutumia vyanzo vya maji kwa kuanzisha Lambo, umwagiliaji kwa njia ya matone pamoja na kuanzisha skimu za umwagiliaji ili kupata mazao mengi.
Kwa upande mwingine amesema Serikali ya Wilaya ya Kigamboni haitawafumbia macho wafugaji wanaopeleka mifugo yao kwenye vyanzo vya maji pamoja na kwenye mashamba ya wakulima na yeyote atakaefanya hivyo basi Ofisi yake haitasita kumchukulia hatua.
Maadhimisho ya siku ya chakula Duniani kwa mwaka 2023 yameongozwa na kauli mbiu isemayo Maji ni uhai, Maji ni chakula, Habaki mtu nyuma
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa