Katibu Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makala amewataka Wananchi wa Manispaa ya Kigamboni kujitokeza na kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia kura linalotarajia kuzinduliwa tarehe 10/10/20224 hadi tarehe 20/10/2024 kwa Mkoa wa Dar es Salaam ili waweze kuchagua viongozi wanaofaa Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27/11/2024
CPA Amos Makala ametoa wito huo leo Agost 27. 2024 katika mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi uliofanyika katika uwanja wa Tungi Mnadani uliopo Kata ya Tungi Manispaa ya Kigamboni.
" Niwaombe kila Mwananchi katika kila Mtaa daftari litakapozinduliwa nenda kajiandikishe ili tarehe 27/11/2024 uwezekupata nafasi ya kupiga kura." Alisema CPA Amos Makala.
Aidha katika Mkutano huo jumla ya kero 65 kutoka kwa Wananchi 47 katika sekta ya huduma ya maji, Barabara, na Ardhi ziliwasilishwa na CPA Makala aliahidi kuzifanyia kazi.
Akijibu baadhi ya maswali ya Wananchi hao Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila amesema zoezi la utiaji wa saini kwaajaili ya ujenzi wa barabara ya Kibada, Mwasonga limeshakamilika na hatua za awali za ujenzi zimeshaanza.
Kwa upande wa huduma ya maji amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia ujenzi wa mabomba yenye urefu wa kilimita 32 uanze kujengewa ili Wananchi waweze kupata nafasi ya kupiga kura na kuchagua viongozi wanaofaa kuleta maendeleo ya Taifa letu
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa