"Mnapokuwa katika Kata zenu nawaomba mtoe elimu kwa Wananchi juu ya ugonjwa wa Corona kwa kuepuka Mikutano na kufuata maelekekezo yanayotolewa na wataalamu wa Afya"
Ni wito uliotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu Ng'wilabuzu Ludigija katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mapenda leo katika Ukumbi wa Manispaa kwa lengo la kupitia taarifa za kutoka kwenye Kata na kupokea taarifa za Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika kipindi cha robo ya tatu katika mwaka wa fedha 2019/2020.
Aidha katika kikao Ndugu Ludigija amewataka Wananchi kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Corona na kuwataka kuelimishana ili kujikinga na ugonjwa huo
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa