"Shule ya msingi Mjimwema ni shule ya mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira ni shule ya kipekee na ni ya tofauti"
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa shirika la just flowers MazaYusuf katika zoezi fupi la upandaji wa miti lillilofanyika shule ya Msingi mjimwema kwa lengo la kuunga mkono juhudi za shule hiyo katika Kuhifadhi mazingira.
Aidha katika zoezi hilo Bi Maza amesema upandaji wa miti katika shule ya Msingi Mjimwema ni mchango wa shirika lake katika kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti pia ni kuikumbusha jamii wajibu wake katika kuhifadhi Miti.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya kigamboni Bwana Juvenalis Mauna amesema ukitaka kuibadili jamii yoyote ni lazima uanze katika hatua za awali, kusudio kubwa la kuitumia shule ya Msingi Mjimwema ni kutoa mfano kwa jamii na kuielimisha njia bora za uhifadhi wa mazingira kwa kuwafundisha watoto angali bado wakiwa wadogo.
Sambamba na hilo amewataka Wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wanaitunza vizuri miti iliyopandwa katika shule yao ili kuwahamasisha wadau wengine wa mazingira na kuthamini mchango uliotolewa na Just Flowers.
Zoezi la upandaji wa miti zilizofanywa na Just flowers ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambayo huadhimishwa tarehe 5 mwezi wa 6 kila mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo , Tumia nishati mbadala kukinga mfumo wa ikolojia.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa