Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokiaji A/INSP Prosper David amewataka wananchi wa Manispaa ya Kigamboni kuwa na utaratibu wa kufanya ukaguzi wa miundombinu ya umeme kwenye nyumba zao kila baada ya miaka mitatu (3) hadi sita (6) ili kujikinga na majanga ya moto yanayoweza kutokea kutokana na tatizo la shoti ya Umeme.
A/INSP Prosper ametoa wito huo leo Septemba 3. 2025 katika mafunzo ya tahadhali dhidi ya majanga ya moto yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa lengo la kutoa elimu ya kuzuia, uokoaji na kujikinga na janga hilo
Aidha amewataka kufuata muongozo wa matumizi ya vifaa vya umeme na gesi uliotolewa na mtengenezaji huku akiwataka kuwa makini na visababishi vya moto ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya vifaa hivyo majumbani.
Akizungunza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mkuu wa Divisheni ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu Ndugu Selemani Kateti amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya tahadhari dhidi ya majanga mbalimbali mahala pa kazi kwa watumishi wa Manispaa ya Kigamboni
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa