Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch. Ng’wilabuzu Ludigija ametoa rai kwa wananchi wa kigamboni kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya matibabu kutoka kwa madaktari bingwa waliopo kwenye kituo cha Afya Kigamboni yatakayoendeshwa kwa muda wa siku nne kuanzia leo Jumatatu hadi alhamisi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa matibabu kutoka kwa madaktari hao bingwa wa wanawake,watoto,upasuaji,mifupa, meno na Koo uliofanyika kwenye kituo cha Afya Kigamboni, Mkurugenzi amesema kuwa uchache wa watumishi wa afya hausababishi wananchi kushindwa kufikiwa kwa kupata huduma za kibingwa kama hizo ndio maana wameamua kuandaa kambi hiyo ambayo itawasaidia wananchi wengi kupunguza gharama , muda na usumbufu wa kufata huduma hizo maeneo ya mbali.
“Niwahakikishie Madaktari hawa ukiondoa utaalamu wao ni wakarimu na wanamapokezi mazuri hivyo ni sahihi kabisa, kwasababu mbali na matibabu tunaamini pia katika mapokezi kama tiba, muamini kuwa matatizo mtakayowapelekea yatapatiwa ufumbuzi”Alisema Mkurugenzi.
Ameongeza kuwa Mhe. Rais amewekeza nguvu kubwa kwenye huduma za afya kwa kuamini kuwa ili Taifa liweze kujenga uchumi bora na imara lazima liwe na wananchi wenye afya nzuri na salama , na Kigamboni kwasababu Serikali imewekeza majengo bora ya afya haina budi kuhakikisha majengo hayo yanatumiwa ipasavyo na kutendewa haki.
Aidha Mkurugenzi amesema kuwa huduma hii ni endelevu ambapo baadaya siku hizo nne kuisha kila wiki kutakuwepo na kliniki ya Madaktari Bingwa na kwamba ushiriki wa wananchi kwenye zoezi hili la siku nne litafungua njia ya kufanya zoezi hilo kuwa endelevu zaidi kutokana na wingi wa wananchi watakaojitokeza.
Mkurugenzi pia ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanajiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii CHF ambayo itawawezesha kupata huduma hizo za matibabu kwa urahisi kwa kuzingatia ugonjwa haupigi hodi na wakati mwingine hujitokeza kipindi ambacho mwananchi anakua hana fedha za kujitibia.
Mganga mfawidhi wa Kituoa cha Afya Kigamboni DK.Julius Nyakazilibe amesema kuwa katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi wameona vyema kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu ya kibingwa kwenye maeneo yao ambapo wapo wagonjwa watakaotibiwa kwa msamaha, kwa bima za afya CHF na NHIF, na watakaochangia gharama kidogo kuwezesha kupata matibabu hayo.
Mratibu wa Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke Dk.Hussein Msuma amesema kuwa wameamua kuunga mkono juhudi za Serikali kwa vitendo kwa kuhakikisha wanasogeza huduma za Kibingwa karibu na wananchi na kuwataka watumie vyema fursa hiyo ambayo wangeweza kuipata mpaka kwa rufaa.
Huduma hii ya matibabu ya madaktari Bingwa Itasogezwa pia kwenye Hospitali ya Vijibweni.
Mkurugenzi akisalimiana na wagonjwa waliofika kupata huduma ya matibabu ya kibingwa.
Mkurugenzi wa Manispaa Arch.Ng'wilabuzu Ludigija kulia akisalimiana na mratibu wa madaktari bingwa Dkt. Hussein Msuma
Mgonjwa akijaza taarifa zake ili akatibiwe
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kigamboni Dkt. Julius Nyakazilibe akizungumza na wananchi waliofika kupata matibabu
baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu
jengo la maabara
Mkurugenzi na viongozi wengine wakikagua maabara iliyosheheni vifaa vya kisasa
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa