Shirika la World Share la nchini Korea Kusini limetoa misaada ya mabegi na vifaa vya kujifunzia katika shule ya Msingi Kichangani iliopo kata ya Pemba Mnazi katika Manispaa ya Kigamboni.
Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo hapa nchini Bi.Nara Kim pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo walifika katika shule hiyo ambapo walijionea hali halisi na kuamua kuanza kwa kutoa zawadi ya mabegi kwa wanafunzi wote 203 kuanzia shule ya Awali hadi darasa la Sita.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kichangani Mwl.Mwinda Ulungu alisema shule yake inakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa nyumba za walimu na vyoo vya Walimu kwani mpaka sasa kuna nyumba mbili tu za walimu na kwa upande wa vyoo hakuna vyoo vya walimu ambapo Afisa Elimu Taaluma aliahidi kulitafutia ufumbuzi pamoja na kuongeza idadi ya walimu kwani mpaka sasa shule hiyo ina walimu Tisa tu kati yao mwalimu wa Kike ni moja.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa