"Ndugu zangu Wananchi wa Kata ya Pembamnazi katika miradi hii ya Sekta ya Elimu, Afya, Barabara, Majina na mengineyo. Tuitunze, tuitumie imeletwa kwetu na Mheshimiwa Rais imeonyesha tija na sisi tuendelee mpaka vizazi vijavyo Viikute Miradi hii."
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo leo October 17.2023 katika ziara yake ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali inayotekelezwa katika Kata ya Pembamnazi.
Aidha DC Bulembo ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wataalamu wa Manispaa ya Kigamboni kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Mwalimu inayojengwa katika shule ya Sekondari ya Pembamnazi yenye thamani ya Tsh Mil 114 ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu. Pia D.C ametoa muda wa wiki 3 kwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigamboni (D.M.O) kuhakikisha majengo ya Maabara, Wazazi na Upasuaji yanaanza kuwahudumia Wananchi
Kwa upande mwingine Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewataka watendaji wa Kata na Mitaa kuacha tabia ya kukaa Maofisini badala yake wafuatilie kwa ukaribu miradi yote inayotekezwa katika maeneo yao ili waweze kupata taarifa na changamoto za utekelezaji wa kila mradi
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM aliyemwakilisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya , Ndugu. Mwinkola amemtaka Meneja wa TANESCO Kigamhoni kuhakikisha wanaharakisha kazi ya usambazaji wa huduma ya umeme katika Mtaa wa Potea kwani katika mitaa yote 67 ni mtaa huo pekee ndio ambao haujafikiwa na huduma hiyo ya umeme
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa