Wakazi wa kata ya Somangila Wilayani Kigamboni wamemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Mbutu kichangani kilichopo kata ya Somangila.
Akiwasilisha shukrani hizo kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo, Shukuru Matimbwa mkazi wa Kichangani amesema kuwa tayari majengo matatu yamejengwa ambapo mawili kati ya hayo ni la Huduma za nje (OPD) na maabara na tayari yamekamilika.
Mkazi huyo pia ametumia fursa hiyo kumuomba Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Halima Bulembo kuona namna bora ambayo idara ya afya inaweza kufanya ili kuwapangia watoa huduma kazi katika kituo hicho kwa kuwa pamoja na hatua nzuri ya ujenzi iliyofikiwa lakini bado hakijaanza kufanya kazi kutokana na changamoto ya ukosefu wa wataalamu wa afya.
Akijibu hoja ya ukosefu wa Watumishi wa afya Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Lucas Ngamtwa alisema ifikapo Oktoba 2023 huduma za wagonjwa wa nje zitaanza na kadri siku zinavyoendelea wataendelea kuboresha ili kutoa huduma ilimzuri zaidi.
Mhe. Halima Bulembo ameendelea na ziara yake ya mtaa kwa mtaa ya utatuzi wa kero za wananchi kwa kata ya pemba mnazi, kisarawe II na leo ameanza kutatua kero kwa wananchi wa Kata ya Somangila
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa