Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba ametangaza kutaifisha viwanja vyote ambavyo havijaendelezwa katika halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Ndg Katemba alisema kuwa mpaka sasa viwanja 3002 vimeshatambuliwa katika maeneo ya Kibada , Kisota na Gezaulole na zoezi linaendelea kutambua viwanja vyote vilivyotelekezwa na wamiliki ili zoezi la kuvimilikisha upya lianze mara moja.
"Ndugu zangu tumekuwa na matukio ya watu kuua na kutupwa kwenye maeneo haya ambayo yanaonekana kuwa mapori, hivyo hatuwezi kuendelea kuona matukio kama haya yanaendelea" aliongeza ndg Katemba.
Uamuzi huo ni kutokana na wamiliki wengi waliomilikishwa viwanja kuanzia mwaka 2006 kutoviendeleza na wengine kubadili matumizi ya viwanja hivyo vya makazi au biashara kuwa mashamba.
Amesema kuwa wale wote wenye viwanja vilivyomilikishwa zaidi ya miezi 36 iliyopita na hawajaviendeleza hata kama wamevilipia umiliki wao utaondolewa na kuwamilikisha watu wengine kwa mujibu wa sheria ya Ardhi na mipango miji namba 4 ya mwaka 1999.
Afisa Ardhi wa Manispaa ya kIGAMBONI bW.Said Salehe akizungumza na wananchi waliofika kwenye kikao hicho.
Mtendaji wa Kata akizungumza kwenye kikao na wananchi waliohudhuria kikao hicho.
Baadhi ya wananchi walioshiriki kwenye kikao hicho.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa