Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa amewataka wamiliki wa hoteli zilizopo pembezoni mwa fukwe mwa bahari kudumisha ushirikiano baina yao ili kuweza kuwaibua wahalifu wanaojificha kwenye maeneo hayo na kuboresha ulinzi na usalama.
Akizungumza kwenye kikao cha wamiliki wa hoteli zalizopo ufukweni mwa bahari leo kwenye ukumbi wa Sunrise Hotel , Mkuu wa Wilaya alisema kuwa ameamua kukutana na wamiliki ili kudumisha ushirikiano pamoja na kujadili masuala ya ulinzi na usalama,uhifadhi mazingira na ulipaji kodi.
Akizungumzia suala la ulinzi na usalama amesema kuwa, kumekuwa na kawaida ya wahamiaji haramu kujificha kwenye maeneo hayo na kufanya vitendo vyakiuhalifu hivyo ni vyema wamiliki kuwatambua watu wao na kuhakikisha wanatoa taarifa pale ambapo wanaona kunamtu hawamuelewi kwa usalama wao na wananchi kwa ujumla.
Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano inapenda wawekezaji na inajitahidi kuboresha miundo mbinu ili kuhakikisha wawekezaji wanakuwa salama hivyo wao pia wanaowajibu kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha mafanikio yaliyokusudiwa yanafikiwa.
Amesema kuwa kila mwekezaji awekeze kihalali na alipe anachostahili kulipa na kwamba Serikali haitamvuilia mwekezaji ambaye atakwepa kodi kwa makusudi hususani wale wanaofanya biashara kinyemela bila kusajiliwa na kwataka kuhakikisha wanalipa kodi ambazo zipo kisheria ili kuepuka adha zinazoweza kuzilika.
"Tozo zinazofahamika kisheria zilipwe kwa wakati kuepuka adha zinazoweza kuzuilika, na huu muone kama ni uwajibikaji kwenu"alisema Mkuu wa Wilaya.
Aidha katika suala la mazingira Mkuu wa Wilaya amesema ni marufuu kuweka uzio kwenye njia zinazoelekea fukweni kwani maeneo yote ya fukwe ni mali ya wananchi hivyo nivyema wakaweka mazingira rafiki yatakayowanufaisha wao kama wawekezaji bila kuwazibia njia wananchi ya kufika maeneo ya fukwe.
Aliwataka pia kuhakikisha tathmini za kimazingira zinafanywa kwenye maeneo yao na kuacha kujenga au kufanya shughuli zozote ndani ya mita 60 kutoka baharini ikiwa ni pamoja na kuboresha mifumo ya maji taka.
Mh.Mgandilwa ametoa rai kwa wamiliki wa hoteli hizo kudumisha ulinzi na usalama siku za sikukuu ambazo wateja wanakuwa wengi kwenye maeneo yao kwaajili ya mapumziko ili kuweka ulinzi madhubuti kwa kuzingatia ulinzi ni jukumu la kila mwananchi na kwamba polisi waliopo hawatoshelezi kuwepo kwenye maeneo yote .
Mwisho aliwataka kama wadau wa uwekezaji kuendelea kutangaza fursa za uwekezaji hususani eneo la ardhi kwani Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni inamaeneo mengi ya ardhi ambayo hayajawekezwa hivyo watu mbalimbali wanakaribishwa kuja kuwekeza.
Mkutano huo ulihusisha wamili wa hoteli wanaotoka kwenye Kata tano za Manispaa ya Kigamboni ambazo ni Somangila,Kigamboni,Mji mwema,Pemba mnazi na Kimbiji ambapo Madiwani na wataalamu mbalimbali kutoka TRA,TCCIA, na ofisi ya Mkurugenzi wameshiriki pia.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa akizungumza na wamiliki wa hoteli zilizopo ufukweni kuhusu masuala ya Ushirikiano, ulinzi na usalama, ushiriki wao kwenye kulipa kodi na uhifadhi wa mazingira kwenye ukumbi uliopo Sunrise Hotel leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.David Sukali akiwaeza wawekezaji wa hoteli umuhimu wa kupima ameneo yao ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa kibali cha ujenzi ,kulipa ushuru wa huduma na kupata leseni za biashara.
Mh. Dotto Msawa Diwani wa Kta ya Kigamboni na Mwenyekiti wa Kamati ya uwekezaji Manispaa ya Kigamboni akisisistiza wafanyabiashara kushirikiana na kuwa wepesi wa kutoa taarifa hususani za kuhalifu na kuhakikisha wanaleseni halali za kufanyabiashara mahali walipo kuepuka adha mbalimbali.
Bw. Elicontrol Mrema Mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA akichangia maada ya ulipaji kodi na umuhimu wa ushirikiano baina ya wafanyabiashara na Serikali.
Meneja wa mamlaka ya mapato Temeke Bw. Gamaliel Mafie akitoa ufafanuzi juu ya elimu huduma zinazotolewa na TRA na kusisitiza umuhimu wa usajili wa hoteli na utoaji kodi pasipo kushurutishwa.
MMoja wa mmiliki wa hoteli akitoa hoja yake kuhusu masuala ya kodi kwenye kikao hicho
Baadhi ya wataalamu na wamiliki wa hoteli za pembezoni mwa fukwe waliofika kwenye kikao wkisikiliza kwa makini.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa