 Posted on: September 22nd, 2020
 
            Posted on: September 22nd, 2020
"Nawasisitiza Mjiepushe na migogoro ya Kisiasa katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu pia mzingatie maadili na kanuni za kazi"
	
	
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu, Erasto Kiwale leo katika kikao kazi cha Walimu wakuu, Walimu wakuu wasaidizi, Wataaluma pamoja na Walimu wa Stores (Ugavi na Manunuzi) kwa shule zote za Sekondari za Manispaa ya Kigamboni kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa
	
 
	
Aidha katika kikao hicho Ndugu Kiwale aliwataka walimu hao kuhifadhi na kuweka vizuri taarifa zote za Miradi ya maendeleo wanayoitekeleza ili kuepuka hoja za ukaguzi.
	
	
Sambamba na hilo naye Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa Ndugu, Nyange Darabu ametoa wito kwa walimu wote wa Sekondari kusimamia taaluma ili kuongeza ufaulu.
	
	
Kikao kazi cha Walimu wakuu, Walimu wakuu wasaidizi, Wataaluma pamoja na  Walimu wa Stores (Ugavi na Manunuzi) kimefanyika kwa lengo la kuchochea ufaulu na utendaji kwa Walimu wa Shule za Sekondari zilizopo Manispaa ya Kigamboni.
	

Mkurugenzi wa Manispaa akitolea ufafanuzi juu ya athari za Migogoro ya Kisiasa
	

	
Mwalimu akiuliza swali katika Kikao kazi
	

	
Baadhi ya Walimu wakipokea maagizo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa
 
                              
                              
                            Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa