Mkuu wa Divisheni ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu Manispaa ya Kigamboni Bi. Tabia Nzowa amewataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari kufuata utaratibu uliowekwa na unaotumika kuwasilisha changamoto zao za kimaslahi ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa haraka.
Mkuu huyo wa Divisheni ametoa agizo hilo leo Juni 27. 2024 katika kikao chake na walimu wa shule za Sekondari, Aboud jumbe, Kidete, Kisota Kibugumo pamoja na shule ya Msingi Kibugumo zilizopo ndani ya Manispaa ya Kigamboni kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za walimu hao wanaofundisha katika shule hizo.
Aidha aliwataka walimu hao kufanya kazi kwa weledi na kuiamini Serikali ambayo imekuwa ikifanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha inazifanyia kazi changamoto zao.
Kwa upande mwingine walimu hao walimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwapandisha madaraja pamoja na kuwapandisha vyeo kulingana na mwaka wa fedha husika.
Divisheni ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu imeandaa utaratibu wa kusikiliza kero za Watumishi ndani ya Manispaa ya Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa umma.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa