Afisa Elimu Msingi Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Gifti Kyondo amewapongeza walimu wa shule za Msingi za Serikali na binafsi ndani ya Manispaa ya Kigamboni kwa juhudi zao za kuongoza ufaulu na kuifanya Manispaa kushika nafasi ya kwanza Kimkoa katika Mtihani wa Darasa la saba mwaka 2024.
Ndugu Gift Kyando ametoa pongezi hizo Disemba 5. 2024 katika hafla fupi ya kuwapongeza walimu hao iliyofanyika kwenye fukwe ya Longoni iliyopo kata ya Kigamboni, Manispaa ya kigamboni.
"Kwanza nianze kuwapa hongera waalimu wote wa wilaya ya kigamboni kwa shule za Serikali na binafsi kiukweli mnafanya kazi kubwa Leo hii tumepata nafasi ya kukutana na kusherekea kazi nzuri mnazofanya za kufaulisha wanafunzi mpaka mnashika nafasi ya kwanza kwa mkoa wa Dar es salaam, niwaomba muendelee kujitoa hivi hivi kufundisha vizuri na kuwapa malezi bora Wanafunzi." Alisema Ndugu Gift kiyando.
Akizungumza wakati wa Sherehe hiyo Afisa Elimu Misingi wa Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni Bw. Ally Almasi amewataka walimu hao kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuhakikisha kila Mtoto wa Kitanzania anapata Elimu bora.
Aidha amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano na Ofisi yake huku akiwaasa kufuata kanuni na taratibu zote za utumishi wa umma
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa