Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu Erasto Kiwale amewataka Wenyeviti wa bodi za shule, Wenyeviti wa Kamati za ujezi pamoja na Wakuu wa shule zote za Sekondari na Msingi Manispaa ya Kigamboni kuzingatia taratibu za manunuzi wakati wa ujenzi wa miradi ya maendeleo.
Ndugu Kiwale ametoa wito huo kwenye kikao kazi kilichofanyika mchana wa leo katika ukumbi wa Manispaa kwa lengo la kuboresha usimamizi wa miradi ya maendeleo kwa shule za Sekondari na Msingi.
Aidha katika kikao hicho amewataka Walimu wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kushirikiana na bodi za shule ikiwa ni njia mojawapo ya kuboresha ujenzi wa miradi katika sekta ya elimu Manispaa ya kigamboni.
Sambamba na hilo naye Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kigamboni Bi. Devotha Mihayo amewataka Walimu hao kuhifadhi vizuri nyaraka za Miradi ya Maendeleo ili kuepuka hoja zisizo za lazima na amewataka kushirikiana na TAKUKURU katika kuijenga nchi.
Afisa utumishi wa Manispaa akiwakaribisha katika kikao wenyeviti wa kamati za ujenzi, walimu Wakuu pamoja na Wenyeviti wa bodi,shule za Msingi na Sekondari
Mkuurugenzi wa Manispaa Ndugu Erasto Kiwale akitoa neno kwa wajumbe wa kikao
Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Kigamboni akiwashauri wajumbe kuweka vizuri nyaraka za manunuzi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa