Picha na matukio yaliyojiri katika sherehe ya kuwapongeza walimu wa shule za Msingi za Serikali na binafsi iliyoandaliwa na Idara ya Elimu Msingi Manispaa ya Kigamboni kwa lengo la kuwapongeza Walimu kwa matokeo mazuri katika mtihani wa Darasa la saba ambapo kwa mwaka 2021/2022 Manispaa ilishika nafasi ya 7 Kitafa na nafasi ya 2 Kimkoa.
Aidha katika sherehe hizo Afisa Elimu Misingi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu. Ally H. Almasi ametoa wito kwa Wazazi/Walezi kushirikiana na walimu ili kuongeza ufaulu zaidi kwa wanafunzi.
Hata hivyo Naibu Meya Manispaa ya Kigamboni Mheshimiwa Stephano Waryoba amewapongeza walimu hao kwa kuwa mashujaa katika sekta ya Elimu na kuwataka kushirikiana na Baraza la Madiwani katika kukuza sekta ya Elimuk
Sherehe hiyo ilihitimishwa kwa zoezi la ugawaji wa tuzo na vyeti kwa shule zilizofanya vizuri pamoja na walimu waliofanya vizuri katika masomo yao wanayoyafundisha
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa