Mkuu wa idara ya Kilimo Bi.Priscilla Mhina amewashauri wakulima wa Manispaa ya kigamboni kulima kwa malengo na kuona kilimo ni kitu kizuri ambacho kinaweza kuwavusha kutoka hatua moja kwenda nyingine ikiwa wataongeza thamani ya mazao yao na kujiunga na vyama vya ushirika vitakavyowawezesha kukopesheka na kutanua wigo wa masoko.
Ushauri huo ameutoa Leo alipokuwa akihitimisha mafunzo ya kilimo cha umwagiliaji, umuhimu wa kujiunga na vyama vya ushirika, matumizi sahihi ya mfumo wa kielekroniki wa Kilimo, na namna kuchakata mazao tangu shambani hadi kufikia sokoni kwenye kituo cha mafunzo kilichopo Geza.
Mhina amewaasa wakulima kuzalisha mazao yanayokidhi afya za walaji kwa kufuata kanuni bora za kilimo na kuacha matumizi holela ya dawa za kunyunyizia mazao hali inayopeleka kupata mazao yasiyo na viwango.
Mafunzo haya ya wakulima wadogo yamefanyika kwa Kata zote za Kigamboni na kuhusisha wataalamu wa kilimo kutoka ngazi ya Kata.
Mtaalamu wa Kilimo Victoria Fisso akielezea namna mfumo wa Kilimo ulioanzishwa na Wizara ya Kilimo unaweza kufanya kazi na kluwasaidia wakulima.
Wakulima wakifatilia kwa makini mafunzo.
Mtaalamu w Kilimo cha Umwagiliaji akitoa elimu kwa wakulima
Mtaalamu wa kilimo akielezea wakulima namna bora ya kuweka bidhaa na upatikanaji wa masoko wa bidhaa zinazotokana na kilimo.
mazao yaliyotokana na kilimo cha ngano na muhogo yakiwa kwenye hatua ya kumfikia mlaji na wakulima walioandaa wakifurahia matokeo ya bidhaa zao.
wakulima na wataalamu wakiandaa bidhaa zilizopikwa na wakulima ikiwa ni sehemu ya mafunzo.
wakulima wakiuliza maswali ya ufahamu kukuza ujuzi wao.
Wakulima wakiendelea kuuliza maswali ya ufahamu kuhusu mashine ya kuchakata muhogo.
Afisa ushirika Wilaya akielezea wakulima umuhimu wa kujiunga kwenye vyama vya ushirika.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa