Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo wameendesha mafunzo ya zao la kilimo cha zao la Mbaazi kwenye Bustani ya Gezaulole kwa lengo la kulitambulisha zao hilo na kuelimisha Wakulima na Wananchi umuhimu wa zao hilo na matumizi yake kwa ustawi wa afya ya binadamu lakini pia kujiongezea kipato.
Mkuu wa Idara ya Kilimo Ushirika na Umwagiliaji Bi. Priscilla Mhina amesema kuwa kupitia Idara yake walionelea ni vyema kulitambulisha zao la mbaazi kwa wakulima wa Kigamboni ili kuwanufaisha wakulima kwa kujiongezea kipato lakini pia kuimarisha afya ya mwili kutokana na faida ya kutumia zao hilo.
Katika mafunzo hayo wakulima waliwezeshwa kujua kanuni za kilimo ikiwemo za uchaguzi wa eneo kwa kilimo cha mbaazi, uandaaji wa shamba, uchaguzi wa mbegu bora, upandaji wa mbegu husani kwa kutumia kitalu cha tray ili kuepukana na vimelea vitakavyoathiri mmea, matumizi sahihi ya mbolea na matumizi sahihi ya Dawa katika ukuaji wa zao la Mbaazi.
Akizungumzia faida ya zao la Mbaazi Afisa Lishe Mkoa wa Dar Es Salaam Bi. Anna Andrew amesema kuwa Mbaazi inasaidia kuongeza damu, kuwapa hamu ya kula watoto wanaosumbua kula,ni zao zuri kwa kushusha pressure na kusaidia watu wanaohitaji kupunguza uzito ikiwemo na kuimarisha misuli ya mwili.
Kwa upande wake Afisa kutoka shirika lisilo la Kiserikali la ADRA , Mama Dinabina amesema kuwa ushirikiano wa Serikali na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ni mzuri kwani unasaidia kuwawezesha wananchi kupata fursa mbalimbali bila gharama yoyote ikiwemo ya zao la mbaazi ambalo limewawezesha kuwanufaisha watu wenye lemavu wa ngozi (Albino).
Teresia Januari ni Mkulima wa Kigamboni ,ameshukuru mafunzo yalitotolewa na kusema kwasasa kipaumbele kitakua ni zao la mbaazi kwani ameshatambua umuhimu wa zao hilo katika kuimarisha afya ya binadamu.
Mafunzo hayo yalikuwa ya siku moja ambapo yalihusisha mapishi ya aina mbalimbali yanayotokana na zao la Mbaazi.
wakulima wakipewa mafunzo ya nadharaia kabla ya kupokea mafunzo ya vitendo
Wakulima wakifuatilia mafunzo ya uoteshaji mbegu kwa kutumia tray.
Afisa Lise Mkoa Bi.Anna Andrew akiwaelezea wakulima umihimu wa zao la Mbaazi kwa afya ya Binadamu.
wakulima wakifuatilia mafunzo ya uoteshaji wa Mbegu za zao la Mbaazi kwa kutumia vitalu vya chini ya ardhi.
wakulima wakipewa mafunzo kwa kuangalia mfano wa mazao mengine.
mafunzo ya matumizi ya dawa za kilimo
Picha ya Pamoja baada ya mafunzo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa