Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Fatma Almas Nyangasa amewataka wananchi wa Manispaa ya Kigamboni kuwa na utaratibu wa kufanya usafi kila siku na si kusubiri hadi usafi wa pamoja wa mwisho wa mwezi.
Mheshimiwa Fatma Almas Nyangasa ametoa wito huo asubuhi ya leo tarehe 29/10/2022 katika zoezi la usafi lililofanyioka katika Mtaa wa Dege Kata ya Somangila ikiwa ni utekelezaji wa Kampeni ya Safisha pendezesha Dar es Salaam.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema kuwa usafi ni swala endelevu na ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha maeneo yote ya Kigamboni yanakuwa safi muda wote.
Kwa upande mwingine Mstahiki Meya wa Mnispaa ya kigamboni Mheshimiwa Ernest Mafimbo amesema kuwa yeye na wakuu wa idara zote pamoja na wakuu wa Vitengo Manispaa ya Kigamboni wameamua kumuunga mkono Mkuu wa wilaya ya kigamboni katika kuhakikisha usafi unafanyika na kigamboni inakuwa safi.
Akiongea kwa niaba ya waanyabiashara wadogo Mwenyekiti wa Machinga Geza Center Bwana Omar Rajab ameupongeza utaratibu wa Mkuu wa Wilaya wa kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi katika kila kata na ameushukuru uongozi wote wa Wilaya ya Kigamboni kwa kushiriki usafi katika maeneo ya wazi.
Wilaya ya kigamboni hufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ikiwa ni utekerlezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Amos Makala la kuhakikisha kuwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi unafanyika usafi wa pamoja.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa