WAJUMBE WA MENEJIMENTI YA MANISPAA YA KIGAMBONI WAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH.SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA KUINUA UTALII
Hayo yamejiri leo 7/8/2022 ambapo wajumbe hao wamefanya utalii wa ndani kwa kwenda kutembelea Mikumi National Park wakiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiongea Mkuu wa msafara huo Bi.Flora Malima ambae ni Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa mara baada ya kutembelea Mikumi National Park amesema wanajisikia faraja Kwa kufanya utalii huu na kuwa sehemu ya wachangiaji wa pato la taifa kwani Kwa kufanya utalii tunachangia kukuza pato la Taifa na kuongeza uchumi ili kuleta maendeleo na kumuunga mkono Rais wetu kwani ni moja ya dhamira yake kuona utalii unakua na kupelekea kunyanyua uchumi wa nchi utakaopelekea maendeleo ya taifa .
Katika huu wajumbe hao wamepata kujua na kujionea mambo mbalimbali ya historia ikiwepo Mbuyu mkubwa wenye umri wa miaka 600 ambao pia ni kivutio kikubwa katika hifadhi hiyo.
Aidha wamaejionea wanyama mbalimbali wakiwepo Simba,tembo,twiga,chui huku kukiwa na hali ya utulivu na usalama wa hali ya juu.
Shime watanzania tuamke sasa na kuunga mkono juhudi za Rais wetu Mh.Samia Suluhu Hassan katika kukuza utalii wetu kwa kutembelea hifadhi zetu kwani kwa kufanya hivyo pia tunakuza pato la taifa.
Mikumi National Park ni moja ya hifadhi zinazopatikana hapa nchini Tanzania ambapo ni hifadhi ya nne Kwa ukubwa ipo katikati ya milima ya Uluguru na Lumango range.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa