Naibu Meya Manispaa ya Kigamboni Mheshimiwa Stephano Waryoba amewataka wajumbe wa bodi za usimamizi wa Vituo vya Afya katika Hospitali na Zahanati Manispaa ya Kigamboni kufanya kazi kwa weledi na kwa kujituma ili kutatua changamoto za kiafya kwa Wananchi.
Mheshimiwa Waryoba ametoa wito huo asubuhi ya leo katika hafla fupi ya uzinduzi wa bodi za usimamizi wa Vituo vya Afya iliyofanyika Hospitali ya wilaya ambapo amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia muongozo wa utekelezaji wa bodi hizo
Kwa upande mwingine Kaimu Mganga mkuu wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu Iddy Kheri amewataka wajumbe hao kuwa wazalendo kwa kubuni vyanzo vipya vya Mapato vitakavyosaidia katika upatikanaji wa vifaa tiba.
Kwa upande wake Mratibu wa Afya jamii wilaya ya kigamboni Bi. Dorice Batulaine amewataka wajumbe wa bodi hizo kuonesha ushirikiano kwa wataalamu wa afya katika vituo wanavyovisimamia na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Bodi za usimamizi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya zimeanzishwa kwa kuzingatia sheria kwa lengo la kuongeza chachu katika utoaji wa huduma za Afya
Mjumbe akitoa mchango wke wa mawazo katika mafunzo
Naibu Meya Manispaa ya Kigamboni akifungua mafunzo ya bodi za usimamizi wa Vituo vya Afya
Wajumbe wa bodi za usimamizi wa Vituo vya Afya wakishiriki katika mafunzo ya usimamizi wa vituo
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa