Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng’wilabuzu Ludigija amewataka wataalamu watakaokwenda kufanya uhakiki wa kaya masikini kwaajili ya utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF awamu ya tatu kipindi cha pili kufaanya kazi kwa uadilifu .
Mkurugenzi amaeyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo mafupi ya uwezeshaji kwa wataalamu wa uhakiki yaliyofanyika Ofisini kwake kwenye ukumbi wa mikutano na kuwaeleza kwamba ni vyema kufuata kanuni na muongozo wa mfuko huo ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa . “ Nawaamini mnafanya kazi vizuri, naomba mfanye kazi kwa uaminifu kuepuka matatizo, fedha zitakazoletwa zifikie lengo na kuleta matokeo, kinyume na hapo tafsiri yake itakua ni matumizi mabaya ya fedha na mimi sipendi tufike huko” alisema Mkurugenzi.
Uhakiki Kigamboni unatatrajiwa kufanyika kwenye mitaa 39 kwa awamu ya kwanza ambayo ipo kwenye mpango wa TASAF, ikumbukwe mradi huuu umelenga kupunguza umasikini kwa kuinua uchumi wa wananchi na kuwekeza kwa watoto hususani kwenye maeneo ya Elimu na Afya.
Mkuu wa Iadar ya Maendeleo ya Jmanii BI.Happyness Luteganya akizungumiza kwa ufupi mradi
Baadhi ya wakuu wa Idara
Mkurugenzi Arch.Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza na wataalamu wa uhakiki Kaya masikini.
Muwezeshaji akitoa elimu kwa wataalamu wanaotakiwa kwenda kuhakiki Kaya masikini
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa