Mkuu wa Wilaya ya kigamboni leo ametembelea wafanyabiashara wa maduka ya vyakula na kuwataka kutumia bei elekezi ya uuzaji wa Sukari ya 2700 rejareja kwa kilo na 2600 kwa jumla baada ya kukubaliana na baadhi ya wafanyabishara jana kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwake .
Mkuu wa Wilaya amewataka wafanyabishara wa vyakula waliokuwa wanauza na Sukari kuendelea kuuza kwa bei elekezi hususani katika kipindi hiki cha ramadhani na kwamba kama maduka yatakua yanauza bidhaa nyingine za vyakula lakini sukari hakuna na yatakayouza kinyume na bei elekezi yatatambuliwa kuanzia kesho tarehe 8/05/2020 na yatafungwa hadi hapo watakaporudisha sukari kwenye maduka yao.
Mhe.Sara amesema kuwa Serikali inapambana kuhakikisha wananchi wanapata sukari na kuuziwa kwa bei ya kawaida katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na changamoto kidogo ya upatikanaji kutokana na baadhi ya meli kuzuiwa sababu ya Corona lakini pia changamoto ya mvua iliyosababisha uzalishaji mdogo kwenye viwanda vyetu kwasababu ya miwa kutohitaji maji mengi.
“ Leo nimewatembelea kuona upatikanaji wa sukari upo vipi na bei mnayouza, sasa katika kipindi hiki cha mpito naomba tusaidiane kutoa huduma ya sukari kwa wananchi , najua hamuwezi kupata faida lakini mitaji yenu haiwezi kukata, hivyo naomba tuuze sukari kwa bei hii tuliyokubaliana mimi nisingependa kutumia nguvu na kufunga madukayenu”Amesema Mhe. Sara
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa