“Kwa niaba ya Manispaa ya Kigamboni napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kutambua mahitaji ya makundi maalumu haswa katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa Corona, pia natoa wito kwa wadau wengine kujitoa katika kuisaidia Jamii.”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu. Ng’wilabuzu Ludigija wakati akipokea msaada uliotolewa leo na Taasisis ya Wanawake wasanifu Majengo uliokabidhiwa na Mwenyekiti wa Taasisis hiyo Mhandisi Victoria Marwa kwaajili ya kituo cha kulea Wazee cha Nunge kilichopo katika Kata ya Vijibweni.
Aidha msaada uliotolewa ni pamoja na Ndoo za kunawia mikono 25, Unga wa sembe kilo 100, Barakoa /Mask 100, Sanitaizer chupa 25, Mafuta ya kupikia lita 60, Toilet paper katoni 10, Ngao za uso katoni 5, Miche ya sabuni 25, Chumvi katoni 1, Maharage kilo 50, Sukari kilo 40, Mchele kilo 200, pamoja na Njugu mawe kilo 50.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa