Wadau mbalimbali wa Manispaa ya Kigamboni wanaojihusisha na mapambano na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI wamekutana leo kwa lengo la kujadiliana namna itakayowezesha kuhakikisha mapambano dhidi ya ukimwi yanafikia lengo la 95 95 95 hususani kwenye makundi ambayo hayafikiwi ipasavyo.
Mgeni rasmi wa semina hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabad Hoja amesema kuwa jamii imejisahau na kuona kuwa janga la ukimwi ni kama halipo wakati hali inaonesha kuwa kwa Wilaya ya Kigambnoni maambukizi ya ukimwi yamezidi kuongezeka kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018 badala ya kupungua.
Ameongeza kuwa ni vyema elimu ikatolewa na wanajamii wote wakaelewa namna bora ya kubadili mifumo yao ya maisha ili kukabiliana na changamoto hii ya kuongezeka kwa maambukizi badala ya kupungua.
Kwa upande wake mratibu wa Virusi vya UKIMWI Wilaya ya Kigamboni Bi.Happy Paschal alisema kuwa Wilaya ya kigamboni maambukizi ya ukimwi yameongezeka badala ya kupungua ambapo waathirika wengi ni wanawake .
Amesema kuwa suala la maambukizi ni letu sote na kwamba elimu inatolewa lakini hamasa ya upimaji kwa jamii bado ni ndogo ukilinganisha na idadai ya watu waliopo , wengi hawajitokezi kupima hususani wanaume ambao huwategea wake zao pindi wanapokuwa wajazito ili kupata majibu ya maambukizi ya UKIMWI.
Kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka 2018, jumla ya watu 45704 wamefikiwa katika upimaji ambapo wanawake ni 28270 na wanaume 17434 na kati yao 25400 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kati yao wanaume 725 wanawake 1329.
Wadau walioshiriki katika semina hiyo ni pamoja na JSI,JHPIEGO,ICAP,DAWATI LA JINSIA ,YOSSADO,KIPENET,KIYODEN,KONGA,CMPD, SAMAI GROUP NA WADAU WENGINE.
Aidha wadau wameshauriwa kushirikiana na kuona kila mmoja anaumuhimu katika mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi na kwamba jitihada kubwa zifanyike kuwafikia wananchi ambao hawafikiwi na wanaishi mbali na vituo vya Afya ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Kigamboni Mhe.Maabad Hoja akizungimza kwenye semina
Wadau wakimsikiliza Kwa makini Mratibu Wa kudhibiti maambukizi ya Ukimwi Wilaya
Baadhi ya wadau wakifatilia mjadala wa namna bora itakayosaidia kudhibiti ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Baadhi ya wadau wakifatilia mjadala wa namna bora itakayosaidia kudhibiti ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Insp.Fatuma kutoka dawati LA jinsia akizungimzia shughuli wanazofanya
Afisa mradi na muwezeshaji kutoka JSI akieleza shughuli wanazofanya katika kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi
Afisa utekelezaji Wa ICAP Bi. Mitha Kenani akielezea shughuli wanazofanya
Emma Olotu Afisa mradi kutoka JHPIEGO akifafanua shughuli wanazofanya katika kudhibiti maambukizi ya Ukimwi na namna wanavyoyafikia makundi mbalimbali
Afisa Ustawi Manispaa ya Kigamboni akielezea umuhimu Wa kuwafikia sober house (Wajidunga madawa) katika kudhibiti na kupambana na maambukizi ya Ukimwi
Mchungaji akielezea namna wanavyoshiriki kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
Mwenyekiti Wa Madereva Bodaboda Wilaya ya Kigamboni akielezeauboreshwaji Wa huduma za upimaji Afya hususan kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa