Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri leo amekutana na kuzungumza na vikundi vya kinamama na vijana kwa lengo la kuwapa elimu na kuwatarifu namna ambavyo vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo vinaweza kuwa dhamana kwenye ukopaji wa mikopo Benki ya CRDB .
Akizungumza kwenye viwanja vya ofisi Mjimwema Mkuu wa Wilaya amesema kuwa baada ya kuona taasisi za fedha zinatoa mikopo yenye masharti magumu , uongozi wa Wilaya na Banki ya CRDB walifanya mazungumzo na kuandaa utaratibu ambao utawezesha wafanyabiashara wadogo wenye vitambulisho vya biashara kupata mikopo itakayokuza mitaji yao.
Mkuu wa Wilaya ameongeza kuwa baada ya kukamilisha zoezi la kugawa vitambulisho vya wafanyabiashara wenye mitaji midogo wameamua kukipa thamani kitambulisho kwani kitawawezesha kuwaondolea bugudha wafanyabiashara wadogo, kupata taarifa zao na kujiunganisha na benki kwa namana bora ya kupata mikopo.
Aidha amesema ili uweze kuwa na sifa ya kukopesheka ndani ya kikundi kama mtu mmoja mmoja ni lazima uwe na kitambulisho cha mfanayabiashara na kuongeza kuwa mikopo itakayotolewa itaanzia laki 1 hadi laki 5 ambapo kwa mkopo wa laki 1 riba itakuwa ni 1500 kwa mwezi .
“Mfumo huu ni sisi nchi nzima ndio tumeuanzisha kwa kutumia dhamana ya kitambulisho kuhakikisha mnakuza mitaji yenu kwa mikopo ya riba nafuu, Nimewaita wanavikundi sababu unamkopesha unayemjua, mikopo inayotolewa na manispaa ile ya asilimia 10 haijitoshelezi ndio maana tumekuja na njia hii mbadala kwa sababu kila mtu atapata pesa yake mwenyewe”
Meneja wa Benki ya CRDB Bw. Samson Keenja amesema kuwa Benki imetenga Bilioni 10 kwaajili ya kuwakopesha wanavikundi wenye vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo ambapo wameweka masharti mepesi yatakayomuwezesha kila mwakakikundi kukopa.
Ameongeza kuwa kwasababu ndio kwanza wanaanza Kigamboni , angependa ingekua ya mfano ili waweze kusambaa na maeneno mengine nchini, ambapo pia Elimu ya kutunza fedha, utunzaji wa kumbukumbu na namna ya kupata mikopo itatolewa kwa wote.
“Uamuzi wa kufanikiwa au kutokufanikiwa ni sisi wenyewe, tumieni fursa hii ili kuinua uchumi wenu kama ambavyo uongozi wa Wilaya unavyowapigania” Alisema Meneja
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri akizungumza na wanavikundi wakinamama na Vijana
Baadhi ya wakinamam na Vijana wakishangilia vitambulisho kuwa dhamana ya Mikopo kwao
Baadhi ya wananwake na Vijana walioshiriki hafla hiyo
Baadhi ya wanavikundi wakinamama walioshiriki hafla hiyo
Meneja wa CRDB Samson Keeenja akizungumza na wamama na vijana taratibu za kutumia kitambulisho kupata mikopo.
Meneja akizungumza na wakinamama na Vijana walioshiriki kwenye hafla hiyo
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa