NA Joseph Aemkiwa
Katibu wa NEC itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Mheshimiwa Sophia Mjema amewataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanasikiliza na kutatua kero za Wananchi wote wanaowahudumia.
Mheshimiwa Mjema ametoa agizo hilo leo katika Mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mheshimiwa Faustine Ndugulile kwa lengo la kuwaelezea Wananchi utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kigamboni.
AIidha amewataka viongozi hao kusimamia vizuri fedha zinazoletwa na Serikali kuu kwaajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo hususani ni barabara zinazojengwa ili kufungua uchumi kwa kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na Wananchi.
"Chama kitaleta viongozi wanaowasikiliza wanachi na wanaowahudumia kwa unyenyekevu, umakini na weledi." Mheshimiwa Mjema alisema.
Kwa upande mwingine Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mheshimiwa Faustine Ndugulile ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa. Dr. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya Mkoa wa Dar es Salaam inayotarajiwa kijengwa ndani ya Wilaya ya Kigamboni.
Pia amewataka Wananchi kuwaamini Madiwani waliowachagua kwani wako kwaajili ya kuwahudumia na kuleta maendeleo ya Manispaa na Wilaya kwa ujumla.
Aidha ameeleza kuwa Ofisi yake imeweka kipaumbele katika ujenzi wa barabara kwani ni changamoto kubwa ndani ya Kigamboni na pia aleeza kuwa ujio wa mradi wa DMDP utasaidia kupunguza adha kwa kiasi kikubwa ambapo Kigamboni imepata 30% ambayo ni kuwa ukilinganisha na Wilaya nyingine
Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mheshimiwa Faustine Ndugulile akieleza utekelezaji wa ilani
Baadhi ya Wananchi walioshiriki katika mkutano wa Mheshimiwa Mbunge
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo akiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa