MANISPAA YA KIGAMBONI KUTOA MIL. 438,111,518.54 KATIKA ROBO YA KWANZA ,VIKUNDI 24 VITAKAVYONUFAIKA VYAPEWA MAFUNZO
Hayo yamebainika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Kigamboni ambapo vikundi 7 vya vijana ,kina vikundi 11vya wanawake na vikundi 6 vya walemavu watapatiwa mkopo wa mil.438,111,518.54 katika Robo ya Kwanza wamepewa mafunzo namna ya matumizi Sahihi ya pesa watakazopewa ili ziweze kuleta tija na faida na kuwawezesha kuzirejesha,lakini pia elimu ya uongozi,fedha,kanuni na sheria mbalimbali za mikopo ya asilimia 10,masuala ya Rushwa, ukaguzi na namna ya kutumia mfumo wa TPLMIS.(mfumo wa malipo ya mikopo ya asilimia 10)
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo kaimu mkuu WA Idara ya maendeleo ya jamii ndg.Aliadina Peter amesema Mafunzo hayo Yana lengo la kuwajengea uwezo katika maeneo mbalimbali ili mikopo wanayopokea uweze kuwa na tija kwao na pia kuweza kutimiza masharti ya mkopo ikiwepo kutumia kwa ombi lililokusudiwa.Lakini pia amewaonya katika suala la marejesho kwani imekuwa tatizo kwa baadhi ya vikundi kutorejesha kwa wakati.
Akiongea akitoa mada ya masuala ya biashara Afisa biashara Nyasama Mohamed ameongelea masharti mbalimbali ya uanzishwaji wa biashara ikiwepo ukataji wa leseni ,ulipaji wa shuru mbalimbali,aidha masuala ya masharti ya kiafya iwapo biashara ni ya masuala ya uuzaji wa vyakula,hivyo amewataka kuzingatia taratibu za kibiashara ili kuepuka faini na usumbufu.
Nae Afisa Ukaguzi wa ndani ndg.Chacha Nyamriba akitoa mada ametoa msisitizo katika suala zima la uwazi katika masuala ya pesa na matumizi sahihi ya matumizi ya pesa kutokana na lengo ikizingatiwa na nyaraja muhimu zinazotakiwa katika masuala yahusuyo fedha ili kuepuka usumbufu wakati wa kukaguliwa.
Kuhusu masuala ya rushwa Afisa wa TAKUKURU Bi. Neema akiongelea masuala ya rushwa amewaelimisha kuhusu Aina za rushwa na madhara yake katika maeneo mbalimbali ikiwepo kuvunjwa kwa haki, migogoro baina ya wana vikundi na hata maradhi kupitia rushwa ya Ngono.Hivyo amewasisitizia kuwa na hofu ya Mungu ili iwaongoze katika kuepuka kujiingiza katika masuala ya Rushwa.
Akifafanua sheria na kanuni mbalimbali za mikopo ya asilimia kumi ya Halmashauri Mwanasheria Bi.Rose Mligo amesema mikopo hii ina kanuni maalum kila kikundi hakina budi kufuata sheria ambapo mikopo yote inasimamiwa na sheria ya mikopo ya asilimia kumi ,aidha mikataba ambayo wanaisaini nayo ina kanuni zake sheria za mikataba,aidha kuna kanuni ya adhabu ambayo hutumika pale ambapo kikundi kimekiuka masharti ya mkopo, Mwanasheria huyo amewasisitizia kuwa wawe makini katika kuhakikisha wanatumia pesa kulingana na maombi na si kugawana pesa kwa wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa juu yao.
Katika suala la uongozi na utawala Bora Afisa utumishi ndg.Cosmas Hinju alitoa elimu kwa wanavikundi hao ambapo moja ya msisitizo aliowapa viongozi wa vikundi nufaika kuwa wao ndio waonyesha njia katika vikundi vyao hivyo inabidi wajitambue,wawe wawazi katika masuala ya kikundi ikiwepo uwazi wa taarifa za mahesabu aidha kuwa makini wa kufanya utafiti kabla ya kufanyia maamuzi yoyote,pamoja na hayo awe ni mwenye kuzingatia sheria za nchi,kuwa wasiri na kila mwanakikundi ajihisi ni sehemu ya mafanikio ya kikundi.
Katika elimu ya fedha Mhasibu wa Manispaa Bi.Yusra aliwaelekeza namna ya kutunza kumbukumbu za fedha za marejesho wanayofanya aidha wawe wafuatiliaji wa madeni yao katika ofisi ya Manispaa ilikuwa na ulinganisho wa taarifa zao,pia walisisitizwa umuhimu wa kutunza risiti mbalimbali za miamala na kuhakikisha akaunti zao za vikundi za benki zinakuwa hai.
Pamoja na mafunzo hayo wamepata fursa ya kufundishwa kwa vitendo namna ya kutumia mfumo wa TPLMIS katika kujisajili na kujaza taarifa zao mbalimbali na hata kutuma maombi ya mkopo na namna ya kufungua email ya kikundi kupitia mfumo huo,mafunzo yaliyotolewa na Afisa Vijana Veronika Kiluvia.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini KGMC
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa