Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kigamboni Bw. Erasto Kiwale amewaasa makatibu wa vyama vya siasa vyenye wagombea kusimamia majukumu yao kwa uaminifu, ili kuepuka lawama kwa kutoa ushirikiano na kuamini kuwa Uchaguzi unaongozwa na miongozo, kanuni na sera hivyo ni vyema kila mmoja akasimamia nidhamu ya mawakala.
Hayo ameyazungumza leo alivyokuwa kwenye kikao cha kujengeana uelewa kilichoandaliwa kwa ngazi ya Wilaya na makatibu wa vyama vya siasa vyenye wagombea ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Manispaa ambapo utimizaji wa wajibu kwa kila mmoja umesisitizwa ili haki iweze kupatikana.
Aidha amewaasa viongozi kuwa chanzo cha utulivu na wawe wa kwanza kutoa elimu kwa wananchi kuwaelezea umuhimu wa kwenda kuwapigia kura viongozi wanaowahitaji kwani Serikali imetumia gharama kubwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na Utulivu.
Aidha Makatibu wa vyama vya siasa wamesisitiza utunzaji wa amani kwa maslahi ya Taifa hususani katika nyakati hizi za kuelekea uchaguzi kwani kunamaisha baada ya uchaguzi ambayo yanawagusa watanzania wote.
Kigamboni inavituo 417 vya kupigia kura kwa kata zote 9 na tayari orodha ya majina imebandikwa kwenye vituo hivyo vya kupigia kura.
Afisa Uchaguzi Kigamboni akitoa maelezo ya idadi ya vituo kwa kila kata na kusisitiza Makatibu kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura.
Baadhi ya Makatibu wa vyama vya siasa vyenye wagombea
Katibu wa chama cha sisasa akitoa maoni na hoja za kuboresha zoezi la upigaji kura
makatibu wa vyama vya siasa
Msimamizi msaidizi wa jimbo akitoa elimu ya umuhimu wa uwajibikaji katika upatikanaji wa haki.
Msimamizi msaidizi wa Jimbo akitoa maelezo ya majukumu ya watendaji wa vituo vya kupigia kura
.
Msimamizi msaidizi wa jimbo akitoa miongozo ya haki ya mwananchi inayomruhusu mwananchi kupiga kura akiwa ndani au nje ya jimbo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa