Uongozi wa Vijana CCM Mkoa wapongeza Halmashauri ya manispaa ya kigamboni kwa kutenga Milioni 240 za mikopo ya vijana zinazolenga kuwainua kiuchumi kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Pongezi hizo zilitolewa juzi walipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni yenye lengo la kuangalia kwa kiasi gani Ilani ya chama cha mapinduzi inatekelezwa na mikakati iiyopo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Bw. Mussa Kilakala alisema kuwa Kigamboni na uchanga wake imepiga hatua kwa kiwango kikubwa sana hata kufikia hatua ya kuwazidi Manispaa kongwe kama Kinondoni ambao wametenga milioni 200 ikiwa na Kata 20 , wakati Kigamboni imetenga milioni 240 ikiwa na Kata 9 tu.
“Kufikia Manispaa changa kuwa mbele ya Manispaa kongwe sio jambo dogo kwakweli mnastahili pongezi, tunawapongeza wataalamu wote, Mkurugenzi, Madiwani na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na ninaamini bajeti ijayo itakuwa kubwa zaidi ya hii na vijana wengi watanufaika” alisema Kilakala
Kilakala alisema kuwa mbali na Manisapa kutenga hizo Milioni 240 na kugawa pikipiki 100 kwa vijana mwezi ujao ikiwa ni kipaumbele cha sasa kwa Manispaa , wakati mwingine iangalie na maeneo mengine ili vijana waweze kufikiwa wote, kwakuzingatia vijana wanajishughulisha na shughuli nyingi kama kilimo, uvuvi na biashara nyingine mbalimbali.
“ Vijana wapo wengi na ndio nguvu kazi ya Taifa ni vyema kuwawezesha kiuchumi, wafikieni vijana wote wa makundi mengine ili wao pia waone thamani ya kuwepo kwenye Halmashauri ya manispaa ya Kigamboni” Alisema Kilakala.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa alipongeza pia Manispaa ya kigamboni kwa kupokea tuzo ya utoaji wa mikopo ya wanawake mwaka jana na kusema kuwa tuzo nyingine inakuja kama manispaa ikitoa vizuri mikopo ya Vijana.
Alishauri pia katika ugawaji wa pikipiki kuwaangalia vijana waajiriwa binafsi wa pikipiki ambao wanakandamizwa na mikataba migumu inayowanufaisha zaidi waajiri na kuwaacha vijana hawana kitu chochote , kwani kuna wimbi kubwa lililopo kwa waajiriwa binafsi ambapo mikataba wanayoingia haina maslahi kwa pande zote mbili.
Kilakala alishauri Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kutumia benki rafiki ili kuondoa malalamiko ya wakopaji , iwe ni sehemu ya kutoa msaada na sio kufanya biashara ili lengo la kuwainua vijana kiuchumi lifikiwe kama lilivyokusudiwa.
Aliongeza kuwa Ofisi ya MKurugenzi na uongozi wa UVCCM Wilaya washirikiane kwa karibu katika kuwatambua vijana watakaonufaika na mikopo hiyo ili iwe rahisi pia kuwafatailia wakati wa urejeshaji wa mikopo hiyo.
Mwisho aliwaomba Waheshimiwa Madiwani kusaidia utambuzi wa vikundi vya vijana wanaotarajiwa kunufaika na mikopo hiyo ili kurahisisha usimamizi na kuweka rekodi nzuri ya wakopaji ikiwa ni pamoja na ushawishi wa urejeshwaji wa mikopo ili kukopesha vijana wengine.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mnispaa ya kigamboni Bw. David Sukali alieleza kuwa Manispaa imejipanga kuhakikisha utaratibu mzuri unawekwa ili kuwafikia vijana wengi na kwamba kwa sasa tayari kampuni ya Bima imeandaliwa kwaajili ya kutoa elimu kwa wakopaji na risk itakuwa ya kampuni na sio mkopaji lengo vijana wainuke kiuchumi.
Halmashauri ya manispaa ya Kigamboni kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ilitenga bajeti ya Milioni 240 kwaajili ya mikopo ya vijana ambapo mpaka sasa pikipiki 100 zipo hatua ya manunuzi na zinatarajiwa kutolewa mwezi wa nne kwa vijana ambapo kila Kata inatarajiwa kupokea pikipiki 5.
Ziara ya uongozi wa UVCCM Mkoa ilianzia ofisi ya Mkuu wa Wilaya na walitembelea miradi ya ujenzi wa kituo cha Afya Kimbiji na jengo la utawala la Manispaa linalojengwa Gezaulole.
Uongozi wa UVCCM Mkoa, wataalamu wa Manispaa ya kigamboni walipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa akielezea histori ya manispaa kwa ufupi ofisini kwake alipotembelewa na uongozi wa UVCCM mkoa.
Katibu wa UVCCM Mkoa Bw. Said Yassin akitoa malezo walipotembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Bw. Mussa Kilakala akipongeza na kushauri Manispaa kuhusu mikopo ya Vijana
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw. David Sukali akifafanua namna ambavyo Manispaa imejipanga kwenye utoaji wa mikopo ya vijana na urjeshaji wa mikopo hiyo.
Baadhi ya wakuu wa idara na vitengo wakifatilia kwa makini maelekezo yanayotolewa na Uongozi wa UVCCM Mkoa.
Katibu wa UVCCM kushoto Bw.Said Yassin na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Bw. Mussa Kilakala wakifatilia kwa makini taarifa ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wakati Mchumi alipokuwa akiwasilisha.
Viongozi wa UVCCM wakifatilia kwa makini taarifa ya utekelezaji ya Manispaa ya Kigamboni.
Mchumi wa Halmashauri ya Manispaa Bw. Maxmillian Manyuka akisoma taarifa ya Manispaa ya Kigamboni
Picha ya pamoja baina ya uongozi wa UVCCM Mkoa , Mkuu wa Wilaya aliyevaa kanzu nyeupe na Kaimu Mkurugenzi
Picha ya pamoja baina ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni aliyevaa kanzu nyeupe, uongozi wa UVCCM Mkoa , Kaimu Mkurugenzi na Wataalam wa Manispaa ya Kigamboni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa