HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI YATOA MIKOPO YA 10% BIL.1,401,252,005.53 KWA MWAKA 2021/2022
Katika kuhakikisha inatekeleza vyema agizo la serikali la kuhakikisha kila Halmashauri inatenga asilimia 10% ya mapato yake ili kutoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wanawake,vijana na walemavu ili waboreshe uchumi na biashara zao.
Kwa mwaka wa fedha WA 2021/2022 Manispaa ya Kigamboni imetoa mikopo kwa makundi yote matatu kama ifuatavyo
Vikundi vya wanawake 52 wamenufaika kwa kupewa Tshs.507,557,637.76 ambazo wametumia kuboresha biashara zao.
Aidha vikundi vya vijana 33 wanufaika kwa kupewa Tshs 626,987,218.77
Vilevile kwa upande wa vikundi vya watu wenye ulemavu vikundi 20 vimenufaika kwa kupewa 266,712,149 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Utekelezaji huu ni muendelezo wa kila mwaka ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imekuwa ikitenga asilimia kumi ya mapato yake kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi hivyo na kuboresha Manisha yao.
Imetolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa