Utekelezaji wa maagizo hayo umeanza kwa timu ya ufuatiliaji kutambulisha mradi na kutoa elimu kwa wananchi maeneo ambapo mradi huu utatekelezwa ,wananchi wameelimishwa kuhusu mradi huu na kuelezwa umuhimu wake• pia jamii wamejengewa uelewa wa pamoja ambapo umefanyika kupitia vikao mbalimbali vilivyohudhuriwa na madiwani na viongozi wa serikali za kata na mitaa kwenye maeneo yenye miradi hiyo ambayo ni katika kata ya Mjimwema,kata ya Vijibweni
Aidha uundwaji wa Kamati za Ujenzi, mapokezi ya vifaa na manunuzi kwa mujibu wa Muongozo wa Force Account umefanyika kikamilifu katika kila eneo la Mradi. Moja ya maagizo aliyoyatoa Mh.Bulembo kwa timu ufuatiliaji ya BOOST ni kuwepo kwa uwazi na ushirikishwaji kuanzia ngazi ya chini kwa wananchi washirikikishwe katika hatua zote zinazohitaji kuwahusisha wao.
Kwa Manispaa ya Kigamboni imepokea 1,156,000,000 ambazo zitatumika kujenga shule mpya mbili kwa shule ya Mjimwema na Kibugumo,vyumba 13 vya madarasa Kwa shule za Vijibweni na na Kisiwani ,ujenzi wa vyumba 2 vya mfano vya darasa la awali na matundu ya vyoo na tayari pesa hizo zimeshaenda kwenye shule husika kwa utekelezaji.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa