Afisa lishe kutoka Manispaa ya Kigamboni Bi. Anna Byashara amewataka Wazazi/ Walezi wa Kata ya Kimbiji kuwapa watoto wao vyakula vilivyowekwa virutubisho ili kuimarisha Afya zao.
Bi Anna ametoa wito huo leo October 9.2023 katika maadhimisho ya siku ya Afya na lishe ya Mtaa yaliyofanyika Kata ya Kimbiji Mtaa wa Ngobanya
Sambamba na hilo Afisa lishe amewataka Wananchi wa Kata ya Kimbiji kuzingatia Mlo kamili wenye makundi yote ya chakula ambavyo ni. Nafaka, mizizi na ndizi mbichi na vyakula vitokanavyo na wanyama, Mimea jamii ya kunde, Mboga za majani, Matunda, Vyakula vyevye mafuta ya mimea, Asali, pamoja na sukari
Katika maadhimisho hayo huduma mbalimbali zilitolewa ikiwepo, elimu na vipimo vya magonjwa yasiyoambukizwa, tathmini ya hali ya lishe, elimu na unasihi wa lishe, utoaji wa matone ya vitamini A na dawa za minyoo, huduma ya macho pamoja na uhamasishaji wa kilimo cha mbogamboga na matunda.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa