Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Sarah Msafiri katika jukwaa la uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi hususan Manispaa Kigamboni ambapo lilifanyika katika ukumbi wa Kibada Gardeni leo kuanzia saa mbili asubuhi.
Aidha katika jukwaa hilo Bi Sarah Msafiri alihamasisha jamii kutumia mikopo ya 10% inayotolewa na Manispaa ya Kigamboni kama sehemu ya mitaji itakayowezesha kuwekeza katika biashara.
Sambamba na hilo Mh. Mkuu wa Wilaya amekabidhi Bajaj 10 na Pikipiki 4 zenye thamani ya Tsh Mil 96.1 kwa vikund 4 ikiwa ni vya walemavu 2 pamoja na vijana vikundi 2 zitakazo wawezesha kujikwamua kiuchumi.
Julwaa la uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi Manispaa ya Kigamboni liliandaliwa ikiwa ni kutoa ushuhuda kwa jamii juu ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dr. John Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka 5.
baadhi ya bajaji zilizotolewa kama Mkopo
Mkuu wa Wilaya na Mgeni Rasmi wa Tamasha Mhe. Sara Msafiri akizungumza na wananchi waliofika kwenye mafanikio ya uwezeshwaji wananchi kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya Mhe Sara Msafiri akizungumza na mmoja ya mwananchi aliyefika kwenye tamasha la mafanikio yauwezeshaji kiuchumi.
baadhi ya Viongozi meza kuu
Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri akikagua baadhi ya bidhaa za wajasiliamali
Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafirir akikata utepe ishara ya utayari wa kukabidhi pikipiki na bajaji kama mikopo kwa vijana.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri akikabidhi funguo kwa mmoja wa kijana mnufaika wa mkopo wa bajaji.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa