wananchi wa Kata ya Kimbiji na maeneo jirani Manispaa ya Kigamboni wataondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufata huduma za afya bada ya ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa kwa sasa kukamilika.
Ujenzi wa kituo cha afya umekuja baada ya kupandishwa hadhi mwaka 2015 kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na vikao vya ndani ya Halmashauri , Madiwani kupendekeza Zahanati ya Kimbiji kupandishwa hadhi kuwa kituo cha Afya ikiwa ni utekekelezaji wa sera ya Wizara ya Afya,ustawi wa jamii, jinsia wazee na watoto ya kuwa na kituo cha afya katika kila kata.
Akizungumza juzi kwenye ziara na Umoja wa Vijana CCM mkoa ya ukaguzi wa miradi ya maenedeleo inayotekelezwa na Manispaa, Kaimu Mkurugenzi Bw. David Sukali alisema kuwa ,kuna zahanati 14 lakini vituo vya afya vya Vijibweni na Kigamboni ndivyo vinavyotegemewa hali inayopelekea wananachi wa Kimbiji kutembea umbali wa kilomita 40 - 45 kufata huduma za afya kwenye vituo hivyo.
Aliongeza kuwa Serikali katika mpango wake wa adhima ya kupunguza vifo vya Mama wajawazito na kuboresha huduma za afya, iliandaa mpango maalumu ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni iliingia katika awamu ya pili ya mpango huo, Mnamo mwezi Disemba 2017 Halmashauri ilipokea jumla ya fedha shilingi milioni mia nne (400,000,000) kutoka Serikalini kwaajili ya utekelezaji.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ilianza kwa ujenzi wa jengo la upasuaji,wodi ya kina mama,maabara na chumba cha kuhifadhia maiti ikiwa ni vipaumbele.
Aliongeza kuwa ujenzi umetumia Mafundi wenyeji “local Fundi” kufanikisha ujenzi huu wa mradi ambapo baada ya taratibu kufanywa walipatikana mafundi 4 na kila fundi jengo 1.
wananchi wameshiriki kikamilifu wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Kimbiji Mh. Muhidini Bunaya aliyewahamasisha wananchi kushiriki nguvu kazi ya kusafisha eneo na kuokota mawe kwaajili ya ujenzi ambapo Diwani alishiriki kwa kutoa roli nne za mchanga.
Aidha wafanyabiashara watatu wa usafirishaji walijitolea mchanga roli moja kwa kila mfanyabiashara na Kiwanda cha Lake Cement kilichopo kimbiji kujitolea bulldoza kwaajili ya kusafisha eneo la ujenzi na kupunguza bei ya mfuko wa saruji kutoka shilingi 11,500 hadi 8,000.
Wakazi wa Kimbiji kwa sasa wameweza kuimarika kiuchumi kwani mafundi na vibarua hawa wanahitaji huduma za malazi, chakula na usafiri hivyo kuwa fursa kwa wakazi wa Kimbiji wanaojishughulisha na biashara za chakula,maradhi na usafiri.
Katika kutekeleza Mradi huu vifaa vyote vya ujenzi vinavyopatikana katika maeneo ya kata ya Kimbiji vilinunuliwa,hivyo kusaidia ukuaji wa biashara katika kata Kimbiji kwa kuongeza mzunguko wa fedha ambapo baadhi ya vifaa Vilivyonunuliwa ndani ya Kata ni Mchanga,kokoto,matofali,vifusi na mawe.
Jengo la Maabara,Upasuaji na la kuhifadhia maiti yamefikia katika hatua ya kupaua na Jengo la kina Mama wajawazito, hatua ya kujenga msingi imekamilika., ambapo hadi kufikia tarehe 30/5/2018 majengo yote yanatarajiwa kukamilika.
Msafara kuelekekea kwenye ujenzi wa majengo ya kituo cha afya kimbiji yanapojengwa.
Kaimu Mkurugenzi akitoa baadhi ya maelezo kwenye jengo la kinamama wajawazito.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi.
Kaimu Mkurugenzi Bw.David Sukali wa mwenye suti ya bluu akionesha baaadhi ya vyumba na matumizi yake kwenye jengo la wakinamama wajawazito.
jengo la maabara na upasuaji likiwa kwenye hatua ya upauaji kama inavyoonekana kwenye picha.
Mafundi wakienedelea na ujenzi wa msingi kwenye jengo la wakinamama wajawazito.
ukaguzi jengo la kuhifadhia maiti.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa