Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ni miongoni mwa Halmashauri zilizofanikiwa kupokea fedha kutoka Serikali kuu za uboreshaji wa vituo vya afya na huduma za afya kwa ujumla.
Kituo cha afya Kimbiji kilipokea fedha kiasi cha milioni 400 kwaajili ya upanuzi wa majengo na uboreshaji wa utoaji wa huduma za afya.
Ujenzi wa majengo mapya kwenye kituo hicho ulianza tarehe 5/2/2018 ambapo ilijumuisha majengo ya maabara, upasuaji,jengo la wazazi na chumba cha kuhifadhia maiti.
Ujenzi wa majengo haya umetumia mfumo wa force account ( Mfumo wa kutumia mafundi wa kawaida wanaopatikana eneo husika badala ya wakandarasi na vifaa vya ujenzi vinanunuliwa kwa bei ya sokoni sio ya zabuni) wanachi walihusishwa moja kwa moja kwa kutumia kamati walizoziunda wenyewe za kusimamia ujenzi na kuhakikisha taratibu za manunuzi zinafuatwa kwa kusimamiwa na wataalamu wa manispaa.
Hadi sasa ujenzi upo kwa 98% na baadhi ya majengo yameanza kutumika kama vile maabara.
Ujenzi wa majengo haya utaweza kuboresha huduma za afya kwa ujumla, kusaidia kupunguza vifo kwa mama wajawazito na watoto, pia kuondoa adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kufata huduma za afya kwenye vituo vingine vilivyopo mbali na makazi yao.
eneo la maabara la awali
Jengo la kupokelea wagonjwa na ofisi za madaktari
jengo la mama na mtoto
jengo la maabara na upasuaji
baadhi ya vitanda ambavyo tayari vimewekwa kwenye chumba cha kulaza wagonjwa
Kitanda cha kujifungilia
Mtaalamu wa maabara akiendelea na utekelezaji wa majukumu yake kwenye chumba cha maabara ambacho tayari kimeanza kutumika.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa