Jumla ya Miradi yenye thamani ya shilingi za Kitanzania Bilioni 229,422,929,552 imezinduliwa na mbio za Mwenge kitaifa katika wilaya ya Kigamboni.
Miradi hiyo inajumuhisha miradi mipya iliyowekewa mawe ya Msingi, iliyofunguliwa pamoja pamoja na mingine ambayo ilizinduliwa ikiwa tayari imeanza kazi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2017 ndugu Hamour Hamad Hamour aliwapongeza viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kigamboni kwa ujumla kwa kuzindua moiradi mingi ambayo ilionekana kuwa na umuhimu mkubwa kwa wananchi wa Kigamboni na serikalia kwa ujumla. Katika risala yake Ndugu Hamour alisistiza wananchi kuitunza miradi hiyo ili iweze kuwa endelevu kwa manufaa ya kizazi cha baadaye.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa alitoa wito kwa wananchi kuzingatia ujumbe wa mwenge ambao ni "SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU" ili kila mmoja aone ni wapi anahusika na kwa namna gani kwani katika uchumi wa viwanda kila mwananchi anayo nafasi kuhiriki akiwa mmopja au kama kikundi.
Pia Mh.Mkuu wa wilaya aliwakumbusha wananchi ya kuwa miradi inayozinduliwa kwa pamoja ni mali ya wananchi hivyo kila mmoja ana nafasi ya kuilinda.
Miradi iliyozinduliwa ni pamoja na Barabara inayounganisha Daraja la Mwl.Nyerere na barabara ya Kibada inayojengwa kwa ushirikiano kati ya shirika la NSSF na serikali kuu, Jengo la kuweka na kukopa cha Tulemane yenye akiba ya zaidi ya shilingi milioni 25,mradi wa ufugaji wa samaki wenye thamani ya shilingi milioni 400 pamoja na Jengo la kutolea huduma ya mama na mtoto katika Zahanati ya kisarawe II.
Miradi mingine ni Kiwanda cha Sruji cha Lake cement , nyumba za walimu 6 katika shule ya sekondari ya Somangila pamoja na jengo la kutolea huduma ya VVU/UKIMWI katika zahanati ya Mji mwema.
Miradi hiyo imetekelezwa kwa ushirikiano wa Manispaa ya Kigamboni,Serikali kuu, Wananchi pamoja na wahisani.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa