Ubalozi wa Kuwait umekabidhi zawadi ya vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni ya Vijibweni vyenye thamani ya shilingi milioni 12 za kitanzania ikiwa ni utekelezaji wa mwanzo wa ushirikiano mzuri baina ya Kigamboni na Taifa la Kuwait.
Akizungumza jana kwenye mapokezi ya vifaa tiba hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Mgandilwa ameshukuru kwa zawadi hizo alizozitoa Balozi wa kuwait ikiwa ni ahadi aliyoitoa alipotembelea Hospitalini hapo wiki mbili zilizopita.
Mhe. Mgandilwa alisema kuwa matembezi ya Balozi wa Kuwait katika Hospitali ya vijibweni yalimfanya kubaini changamoto ya baadhi ya vifaa, hivyo kuahidi kurudi kabla ya mwezi wa ramadhani kuisha.
Aliesma kuwa Kuwait na Tanzania ni marafiki na kuna kila sababu ya kuendelea kusapotiana na kudumisha urafiki uliopo huku akimuomba Balozi wa Kuwait kuendelea kusaidia baadhi ya vifaa ambavyo ameahidi atavileta kama vile vitanda vya kung'olea meno vitakavyosaidia kuboresha huduma za afya kwa ubora zaidi.
"Naomba usiishie hapa kwa chochote utakaachona unaweza kusapoti kwenye sekta hizi tatu usisite kutusaidia na mimi kama Mkuu wa Wilaya naahidi kudumisha urafiki wetu" Alisema Mkuu wa Wilaya.
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem alisema zawadi alizozitoa ni mwanzo wa ushirikiano mzuri uliotokana na mapokezi mazuri aliyoyapata kipindi chote kutoka kwa Mkuu wa Wialaya ya Kigamboni pindi alipotembelea Wilayani kwake.
Aliongeza kuwa Ubalozi wa Kuwait umetoa Vitanza 3 vya watoto, vitanda3 vya kujifungulia kinamama, mashine za oksijeni, mabeseni 8 ya watoto waliozaliwa , mashine ya kutolea uchafu pindi mtoto anapokunywa maji machafu wakati wa kujifungua na vifaa vingine ili kuboresha huduma za afya zinazotolea na Hopsitali ya Vijibweni.
Balozi Jasem aliongeza kusema kuwa ataangalia namna atakavyoweza kusaidia kutoa mashine za moyo zilizoombwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na kuahidi kuendeleza ushirikano uliopo na Kigamboni na Tanzania kwa ujumla.
Aidha alisema kuwa Kuwait ina mpango unaojulikana kama Kuwait Blood Bank yenye lengo la kutunza damu salama hivyo atajitahidi kuhakikisha Kigamboni inakua miongoni mwa wanufaika wa mpango huo hususani Hospitali ya Vijibweni ambapo viataletwa vifaa vitakavyotumika kuhifadhia damu salama kwaajili ya kuokoa maisha ya Wananchi wa Tanzania.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe.Hoja Maabad alimshukuru Balozi wa Kuwait kwa zawadi alizozitoa na kumuomba kuendeleza urafiki na ushirikiano mzuri ulioanzishwa kwa manufaa ya wote.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Hashim Mgandilwa kushotoakipeana mkono na Balozi wa Kuwait Mhe.Jasem Al-Najem ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya moja ya mshine alizozitoa.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni kushoto Mhe.Hashim Mgandilwa akipokea zawadi ya Beseni kutoka kwa Balozi wa Kuwait Mhe.Jasem Al-Najem.
Balozi wa Kuwait Mhe.Jasem Al-Najem akimkabidhi zawadi ya beseni mwanamama Olivia Jelard kutoka Ungindoni, Mkuu wa Wilaya Kushoto na Mstahiki Meya Kulia wakishuhudia.
Baadhi ya mabeseni na vifaa vyake yaliyokabidhiwa kwa wamama waliojifungua watoto Hospitali ya Vijibweni
Baadhi ya Vifaa Tiba Vilivyokabidhiwa na ubalozi wa Kuwait
Balozi wa Kuwait Mhe. Jasem Al-Najem akiwa amembeba mmoja wa watoto waliozaliwa siku chache kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni ya Vijibweni, Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na Mganga Mkuu .
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa