Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri pamoja na wataalamu wa Manispaa ya Kigamboni wakiongozwa na Mkurugenzi Arch.Ng'wilabuzu Ludigija leo wamekutana na wataalamu kutoka Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO) kwa lengo la kuanisha maeneo ya uwekezaji ili TIRDO waisaidie Manispaa katika suala zima la kuyatangaza na kutafutia wawekezaji.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kumekua na changamoto ya mabadioliko kwa maana kasi ya utendaji wetu tofauti na ya Mhe. Rais hivyo ni vyema tukajitahidi kwenda kwa speedi nzuri ili tuweze kwenda vizuri kwenye malengo ya Kimanispaa na Kitaifa kwa ujumla wa kujenga Tanzania ya Viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng'wilabuzu Ludigija amesema kuwa Kigamboni inawahitaji na kuwaomba TIRDO waisaidie kutangaza na kuipata wawekezaji kwasababu fursa ya viwanda inaweza kuonekana zaidi kwa vitendo Kigamboni ukilinganisha na maeneo mengine sababu maeneo mengi bado hayajaendelezwa.
Maeneo ya uwekezaji ambayo yameanisha Wilaya ya Kigamboni yapo kwenye sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi,Mazingira,Ardhi na Mipango miji ambapo jumla ya Michoro 85 katika kata mbalimbali imeshaainishwa na jumla ya viwanja 6,320 vimepimwa kwaajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na maeneo muhimu ya taasisi za Serikali,eneo la ofisi za Mkurugenzi, ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Hospitali ya Wilaya ambao ni mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri akieleza dhamira ya kuwahitaji TIRDO katika kuinua Sekta ya Uwekezaji na Tanzania ya Viwanda Wilayani Kigamboni.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Uchumi Bw.Kalila King akiwasilisha maeneo ya Uwekazaji yaliyoanishwa ndani ya Manispaa ya Kigamboni.
Baadhi ya Wataalamu wa Manispaa ya Kigamboni wakifatilia kwa makini uanishwaji wa maeneo ya uwekezaji.
Baadhi ya Wataalamu kutoka TIRDO walioshiriki kwenye kikao cha uanishaji wa maeneo ya uwekezaji Kigamboni.
DR.Lugano Wilson Mkurugenzi wa maendeleo kutoka TIRDO akieleza namna walivyoyapokea maeneo hayo ya uwekezaji na namna mchakato wa ushiriki utakavyoanza
Mkuu wa Idara ya MifugoManispaa ya Kigamboni,Bw. Aaron Bullu akitoa ufafanuzi wa fursa za uwekezaji zilizopo kwenye sekta ya Mifugo
Mkuu wa Idara ya Mazingira na Usafishaji Bw.Sixbert Kyaruzi akifafanua fursa ilipo kwenye sekta ya mazingira na namna ambavyo Manispaa imejipanga kukabiliana na changamoto
Afisa Mipango Miji Kigamboni Bw.Yona Nsenyi akielezea fursa zilizopo upande wa mipangomiji .
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa