Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa utekelezaji wa Ilani wa chama cha Mapinduzi na kusema kuwa ameiona thamani ya fedha katika miradi yote aliyoitembelea hivyo mshikamano uliopo uendelezwe.
Amayezungumza hayo jana mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi aliyoifanya Manispaaa ya Kigamboni yenye lengo la kuona ni namna gani Ilani ya Chama inatekelezwa.
Akizungumza na watumishi na wananchi wanao shiriki kusimamia miradi Bi.Kamba amesema kuwa, Miradi yote inatekelezwa katika ubora na ndani ya wakati na thamani ya fedha ( Value for money) inaonekana.
"Miradi yenu mizuri na inatekelezwa kwa ubora na wakati, mnaspidi nzuri sana hii inaonesha ni naman gani mnaushirikiano, Kigamboni ni Wilaya changa lakini mambo mnayofanya mnawazidi hata Wilaya kongwe, tumependa" Alisema Kamba
Aliongeza kuwa ameona ushirikishwaji katika utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba jamii imeshiriki kikamilifu hali inayopelekea kuona wanao wajibu wa kutunza na kusimamia miradi yao ndio maana wameweza hata kufikia makubaliano ya punguzo la bei ya ununuzi wa vifaa vinayohitajika kwenye ujenzi miradi.
Aidha Bi. Kamba alisema kuwa sheria ya manunuzi inagharimu sana utekelezaji wa miradi , urasimu mwingi tofauti na utaratibu wa mafundi wenyeji unaosaidia kutumia fedha kidogo na miradi kujengwa kwa wakati huku thamani ya fedha ikionekana.
Kamba aliwataka watumishi kuona wanao wajibu na sehemu yao kufanya kazi na kuhudumia wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani na kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa kiwango cha juu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa alisema kwamba yeye pamoja na Madiwani , Mkurugenzi na watendaji wake wanaimba wimbo mmoja , thamani ya fedha inayoonekana katika kila mradi ni matokeo ya usimamizi uliopo ambao wamepewa na mamalaka kusimamaia.
Ameongeza kuwa kigamboni inaweza kuwa ya kwanza kwa Halmashauri zinazotekeleza ujenzi wa makao makuu tangu kuanzishwa kwani ndani ya kipindi kifupi cha miaka 2 tangu kuanzishwa kwake, watumishi watakuwa tayari kwenye jengo lao la Utawala lenye ghorofa 3, hii imewezekana kutokana na mfumo mzuri wa matumizi ya fedha.
Aidha alisema kuwa mfumo unaotumika wa mafundi wenyeji unaokoa kiwango kikubwa cha fedha ambazo zilikuwa zinapotea bila sababu katika mfumo wa manunuzi.
"Nadhani tuendelee kuangali hizi sheria za manunuzi, zinazumiza sana Serikali na tuanze kufuata taratibu za kawaida, mfano mfuko wa misumari kwa mfumo wa manunuzi unaweza nunua hadi elfu 6000, wakati kawaida unanunua elfu3000 hadi elfu 3500"Alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw. Stephene Katemba alishukuru kutembelewa na viongozi wa CCM na kuona namna gani Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa.
Alisema hadi sasa ameshapokea Bilion 2 kwaajili ya ujenzi wa jengo la utawala na taratibu zote zimezingatiwa za kupata mkandarasi , mradi unayobond ya kulinda( secured bond) ikitokea mkandarasi ameshindwa kuendelea na kazi na performance bond ( fedha zitekelezwe kwa kadri inavyotakiwa).
Mwisho aliwakaribisha tena viongozi wa Chama na kwamba kwake ni hamasa kubwa hivyo yeye kama kiongozi atajitahidi kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa kadri ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyotaka.
Ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa iliyoambatana na viongozi mbalimbali wa Chama ilipata fursa ya kutembelea mradi wa ukarabati wa Zahanati ya Buyuni, Ujenzi wa kituo cha Afya Kimbiji, Ujenzi wa miundombinu ya Shule kwaajili ya kuanzisha kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari Nguva, ujenzi wa jengo la utawala na ujenzi wa uanzishwaji Sekondari eneo la Shule ya Msingi Kigamboni.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bi. Kate Kamba akizungumza na kutoa pongezi zake kwa Manispaa ya Kigamboni.
Baadhi ya Wakuu wa idara na vitengo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa alipokuwa akizungumza nao.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani jana kwenye ukumbi wa Mkikutano uliopo shule ya Msingi Mjimwema
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigamboni Dk.Charles Mkombachepa akitoa maelekezo ndani ya jengo la maabara na upasuaji
Mkurugenzi Mwenye suti nyeusi Bw.Stephen Katemba akiongoza msafara kwenda kukagua majengo ya kituo cha afya Kimbiji
Msafara kuelekea jengo la kuhifadhia maiti
jengo la wamama wajawazito likiwa kwenye hatua ya renta
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bi. Kate Kamba akiambatana na viongozi wengine walipotoka kukagua jengo la wamama wajawazito.
Jengo la maabara na upasuaji likiwa katika hatua ya upauaji kama inayoonekana katika picha
Mkurugenzi wa Manispaa aliyenyoosha mkono Bw. Stephen Katemba akifafanua kuhusu mandhari ya Hospitali yatakavyokuwa ,mara baada ya kumalizika ujenzi , hapo ni mbele ya jengo la kuhifadhia maiti.
muonekano wa jengo la kuhifadhia maiti
Muonekano wa nje wa moja ya maabara ya Kisayansi iliyopo Shule ya Sekondari Nguva
muonekano wa moja ya maabara ya kisayansi Shule ya Sekondari Nguvu inayotarajiwa kuwa na kidato cha 5
muonekano wa ndani wa bweni la wanafunzi watkaoanza kidato cha 5
Moja ya chumba ndani ya bweni watakacholala wanafunzi wa kidato cha 5
Mkurugenzi mwenye suti nyeusi akionesha ramani ya jengo la utawala kwa Mwenyekiti wa Mkoa CCM alipotembelea kuona hatua ya ujenzi ilipofikia.
Hatua ya ujenzi jengo la Utawala ilipofikia hadi sasa
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi na viongozi wengine walipotembelea kuona mradi wa ujenzi shule ya sekondari itakayokuwa karibu na shule ya Msingi Kigamboni
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba akishukuru uongozi wa CCM kutembelea miradi na kuona utekelezaji wa Ilani.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa