Waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof Makame Mbarawa ameagiza wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) kuandaa mpangokazi wa kuvifanyia matengenezo vivuko vinavyotoa huduma katika eneo la Feri
Prof. Makame Mbarawa ametoa agizo hilo asubuhi ya leo katika ziara ya kutembelea na kukagua vivuko vinavyotoa huduma kati ya Wilaya ya Kigamboni na Wilaya ya Ilala ambapo alijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na TEMESA haswa katika upande wa vivuko na amewataka kusaini Mkataba na Sangoro Marine ambaye ni Mkandarasi anaefanya ukarabati wa kivuko cha Mv Kazi kwa muda wa wiki 4 ili kivuko hicho kiweze kurejeshwa na kuendelea kutoa huduma kama awali.
Aidha amemtaka Mkandarasi (Sangoro marine) kuhakikisha anafanya kazi kwa kuzingatia muda uliowekwa ili kupunguza adha kwa Wananchi wanaotumia Vivuko hivyo
Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Fatma Almasi Nyangassa amempongeza Mheshimiwa Waziri kwa kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali katika Vivuko hivyo na ameeleza kuwa uwepo wa Vivuko vyevye uhakika ni muhimu sana haswa kwa wakazi wa Wilaya ya Kigamboni ambao hutegemea vivuko hivyo katika shughuli zao za kila siku.
Sambamba na hilo Meneja wa matengezo ya vivuko kutoka TESEMA bwana Lukombe King'ombe ameeleza kuwa mkataba wa matengezo ya MV Kazi utasainiwa siku ya ijumaa tarehe 01/04/2022 na utagharimu kiasi cha Tsh Bilioni 4.5 hadi kukamilika kwake
Aidha Mkurugenzi mtendaji wa Sangoro Marine bwana Meja Sangoro amesema kuwa matengezo ya kivuko hicho yatahusisha ununuzi wa injini mpya, kubadilisha mabati yaliyooza, mfumo wa umeme na maji, pamoja na kupaka rangi na ameahidi kukamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa.
Eneo na Feri linahusisha vivuko 3 ambapo vinavyotoa huduma kwa sasa ni 2 baada ya kivuko kimoja kuvuliwa kwa lengo la kufanyiwa matengezo, aidha Serikali ya awamu ya sita kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imetenga bajeti ya kununua kivuko kikubwa cha 4 chenye uwezo wa kubeba watu 3,000
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa